HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 21, 2023

MASOUD DJUMA AKIRI UGUMU CAF CL

Na John Marwa

KOCHA Mkuu wa KMKM ya Visiwani Zanzibar,  Masoud Djuma amesema bado ana kazi kubwa ya kufanya kwenye safu yake ya ushambuliaji kuelekea mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St George ya Ethiopia.

Amesema hayo baada ya mechi ya kwanza kupoteza nyumbani kwa kichapo cha mabao (1-2) mchezo uliopigwa juzi uwanja wa Azam Complex huku wakitarajia kurudiana Agosti 27, katika dimba la Abebe Bikila, Ethiopia.


Masoud amesema kuna mambo mawili ambayo yaliwaangusha kwenye  mechi ya kwanza ikiwemo kushindwa kutumia nafasi nyingi walizozitengeneza kwa wachezaji wake kukosa uzoefu wa michuano ya kimataifa.

Amesema suala la ushambuliaji analifanyia kazi kwa kuhakikisha wachezaji alionao wanaweza kumpa kitu katika mchezo wa marudiano dhidi ya St George kwa kuweza kufunga idadi kubwa ya mabao.

‘Tunawakosa washambuliaji wetu wako wanne hawana kibali (ITC), tumelazimika kubadilisha baadhi ya wachezaji kuwa wafungaji, nalifanyia kazi safu hiyo kwa kuwaongezea mbinu ili kupata matokeo mazuri mechi yetu ya marudiano.

"Naamini haitakuwa mechi rahisi ninaimani kubwa na wachezaji wangu kubadilisha matokeo dhidi ya St George baada ya kipindi cha pili kucheza vizuri na kutawala mchezo,” alisema Masoud.

Aliongeza kuwa anamatarajio makubwa ya kuvuka hatua hiyo ya awali kwa kufanya vizuri mechi hiyo ya maruadiano ambapo anaamini anaweza kupata matokeo chanya ugenini.



No comments:

Post a Comment

Pages