HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 12, 2023

TISA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA IRINGA

JESHI la Polisi Mkoa wa lringa  linawashikiria watuhumiwa 9 kwa tuhuma mbalimbali za kuvunja na kuiba maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Akizungumza na wanahabari mkoani hapa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi  alisema katika kuimarisha ulinzi na usalama limeendelea kufanya doria na misako mbalimbaii yenye lengo la Kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu mkoani hapa mbapo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao  na mali mbalimbali ambazo ziliibwa.


Alisema kuwa katika Operesheni iliyofanyika kuanzia Julai 7, 2023 hadi Agosti 10 mwaka huu jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa (09) wa makosa ya kuvunja na kuiba ambao ni Samweli Malila (24) mkazi wa kinyanambo C Mafinga, Fahamu Msisi (40) Mkazi wa Mjimwema Mafinga, Acheni Mwinuka (30).
Aliongeza kuwa wengine ni , Satilin Ngoyigange (30) mkazi wa Luganga, Satoki Sanga (50) Mkulima na mkazi wa Luganga, Steven Peter (43) mkazi Mafinga, Said Degela (24) mkazi wa mwangata, Joshua Elihuruma (24) mkazi wa Kitanzini na Goodluck Mpangile (25), mkazi wa Ipogoro

Aidha, Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni Pikipiki nne (04) MC.473 AAP na MC.294 DPG zote aina ya Haoujue, Pikipiki aina ya SUNLG namba na Pikipiki ya matairi matatu MC.724 DHJ 

Alisema Vitu vingine vilivyokamatwa ni TV moja aina EVVOLI, LAPTOP Moja aina ya SnSV, Jeki moja ya  vitu vingine mbalimbali.
 
Kamanda Bukumbi alisema kuwa watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. 



No comments:

Post a Comment

Pages