Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga akikabidhi baadhi ya vifaa vya shule kwa Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii Jane Mwalwembe.
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKURUGENZI
wa Volunteers for Community Development, Justin Nyamoga ametoa msaada
wa vifaa vya shule kwa taasisi ya kijamii ya Sauti ya Jamii kwa ajili ya
watoto wenye huitaji.
Nyamoga ambaye ni mbunge
wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa ametoa msaada huo baada ya kupata
maombi kutoka kwa Mkurugenzi wa Sauti ya Jamii kuhusu kampeni ya Mpe
Kalamu asome ambayo inahusisha watoto wenye uhitaji.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo Nyamoga alisema kwamba lengo ni
kusaidia jamii katika kuwaondolea changamoto mbalimbali zinazowakabili
hivyo msaada huo utakuwa kuwakomboa wanafunzi kwenye masuala ya elimu .
"Taasisi
itakuwa na lengo la kujitolea kwenye masuala mbalimbali ya kijamii
katika kuleta maendeleo hivyo umuhimu mkubwa ni kujitolea kwa nguvu kazi
na Kwa kushirikiana na wadau mbali mbali ndani na nie ya nchi"Alisema
Aliongeza
kuwa msaada huo umekuja wakati ambao watoto wengi wanakosa vifaa
mbalimbali vya elimu hivyo utakuwa mkombozi hata kama kwa uchache
Nyamoga
alikibidhi madaftari , penseli, peni, rula na vifutio kwa taasisi hiyo
na kupokolewa na Mkurugenzi wake Jane Mwalwembe ambaye ni mwanaharakati
wa kupambana na ukatili wa kijinsia mkoa wa Iringa.
Kwa
Upande wake Mwalwembe alishukuru msaada huo kutoka kwa Volunteers for
Community Development kuwa umekuja kwa wakati mwafaka na utawafikia
watoto wenye uhitaji katika shule mbalimbali mkoani Iringa.
Alisema
kuwa Sauti ya Jamii imeanzisha kampeni ya Nipe Kalamu Nisome ikiwa na
lengo la kuwapatia mahitaji watoto wenye uhitaji vifaa vya shule.
No comments:
Post a Comment