Na John Marwa
Haujaisha mpaka iishe. Unaweza kuelezea hivyo kuelekea mchezo wa leo wa marejeano wa Ligi ya Kandanda ya Afrika (AFL) ambapo Miamba ya soka Al Ahly wanawakaribisha Simba SC kwenye Dimba la Ciro International kumsaka mwana nusu fainal wa kwanza wa AFL katika makala haya ya kwanza.
Simba na Ahly walitoshana nguvu kwa sare ya mabao mawili kwa mawili siku tatu zilizopita kwenye mchezo wa ufunguzi wad michuano hiyo yenye ukwasi mkubwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Leo ni ama jasho ama damu hadi Mwamba mmoja apatikane wa kusonga hatua ya nusu fainal jambo ambalo linaufanya mchezo huo kuwa mgumu uukiachilia ugumu na ushindani uliopo wa Miamba hiyo ya Soka Barani Afrika kwa miaka ya hivi karibuni.
Ahly ambao ni wenyeji wanahitaji kushinda ama kupata suluhu ama sare ili kusonga hatua inayofuata huku Mnyama Simba akihitaji kushinda ama kupata sare ya mabao matatu na kuendelea ama mabao mawili kuupeleka mchezo kwenye mikwaju ya penati.
Timu zote mbili hazina cha kupoteza kwenye mchezo wa leo jambo linaloashiria kuwa mbungi itapigwa na ulumbi utamwagika pale kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema ameiandaa timu yake kwenda kuonyesha sanaa ya mchezo wenyewe kwa anaamini mpira wa miguu kwake ni sanaa na sio ukubwa wa timu.
No comments:
Post a Comment