HABARI MSETO (HEADER)


October 24, 2023

WANANCHI WAKWEA KILELENI WAKIICHAPA AZAM FC

Na John Richard Marwa


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL, Yanga SC wamekwea kileleni mwa msimamo wa Ligi mara baada ya kuwaadhibu Azam FC kwa kichapo cha mabao (3-2) mtanange uliounguruma katika Dimba la Benjamin Mkapa.



Ulikuwa mchezo wa Nguvu kwa timu zote kushambuliana kwa nyakati tofauti. Stephanie Azizi Ki amekuwa chuma tatu muhimu katika mchezo huo na kuifanya Yanga kuondoka na alama tatu muhimu.


Iliwachukua Wananchi dakika nane kuweka mpira kambani huku Azam FC wakirejesha bao hilo dakikA ya 18 na kuupeleka mchezo huo mapuziko kwa sare ya bao (1-1).


Kipindi cha pili Azam walerejea kwa kasi na kujipatia bao la pili kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Prince Dube, bao hilo halikufua dafu kwani Azizi Ki aliwarejesha Wananchi mchezoni kwa mpira wa adhabu ambao mlinda lango wa Azam FC alijifunga mwenyewe kisha Azizi Ki akahitimisha shughuli kwa bao la tatu na kuipatia Yanga point tatu muhimu kwenye derby hiyo ya Dar es Salaam.


Kwa ushidi huo Yanga imekwea hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi wakifikisha pointi 15 sawa na Mnyama Simba, Yanga akiwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.


Wananchi wamefunga mabao 18 kwenye michezo sita sawa na wastani wa mabao matatu kila mchezo huku wakiruhusu mabao manne. Wakati huo Simba wakiwa wamefunga mabao 14 na kuruhusu manne lakini Yanga wakiwa na mchezo mmoja zaidi ya Simba.


No comments:

Post a Comment

Pages