Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Aldof Mkenda (kushoto) akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB ,Ruth Zaipuna alipomtembelea waziri huyo ofisini kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ,Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB ,Ruth Zaipuna alipoongoza ujumbe wa NMB kutembelea wizara hiyo Jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Songea
BENKI ya NMB imekabidhi madawati yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25 kwa shule sita mkoani Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya benki hiyo ya kuchangia uboreshaji wa sekta ya elimu nchini.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule za msingi Kiburangoma, legele, lipuma Londoni na Mkuzo za Manisapaa ya Songea pamoja na Shule ya Msingi Mateteleka ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kiburangoma jana, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini Faraja Ng’ingo alibainisha kuwa msaada huo pamoja na kuboresha mazingira ya wanafunzi kujisomea unalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya Elimu.
Ng’ingo alibainisha kuwa Sekta ya Elimu ni miongoni mwa vipaumbele vya benki hiyo katika mkakati wake kabambe wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSI) huku akisisitiza kuwa ni Benki ya NMB itaendela kushirikiana na wadau wote ikiwemo Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii wanayoihudumia.
“Sisi kama benki ya NMB tunaamini kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Kwa kulitambua hili, sekta ya elimu ni miongoni mwa vipaumbele vyetu na kwa miaka mingi sasa tumekuwa tukijitoa kuchangia maboresho ya sekta hii muhimu. Nina furaha kuwa leo tunakabidhi madawati kwa shule sita mkoani Ruvuma na nimatumaini yangu kuwa msaada wetu utakuwa chachu ya ufaulu kwa shule hizi sita,”alisema .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza benki ya NMB kwa msaada huo mkubwa kwa wananchi wa Ruvuma.
Kanali Thomas alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga miundombinu muhimu ya sekta za elimu na afya na kuwapongeza wadau wengine ikiwemo benki ya NMB kwa kujitokeza kuunga mkono jitohada za Serikali.
"Huu ni mfano wa kuigwa. Natumia fursa hii kuipongeza benki ya NMB ya kuendelea kuchangia shughuli za maendelo za Serikali. Natoa rai kwa wadau wengine mkoani Ruvuma kuiga mfano huu wa kuchangia maendeleo," alisema.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile aliishukuru banki ya NMB kwa kupunguza changamoto ya madawati na meza katika shule za msingi na sekondari Manispaa ya Songea.
Alibainisha kuwa katika shule za msingi zilizopo Manispaa ya Songea kuna upungufu wa madawati 5,863 huku shule za sekondari za Manispaa ya Songea zikiwa na upungufu wa meza 6,600.
No comments:
Post a Comment