HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 23, 2024

Nathwani na Sangita mahakamani madai ya kwa kujeruhi jirani

 

Na Mwandishi Wetu

KESI inayowakabili Bharat  Nathwani (57), maarufu kama Chiku na mkewe Sangita Bharat Nathwani (54) imepigwa kalenda hadi Februarri 19, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa dhidi ya mashitaka manne ikiwamo kujeruhi na kutoa lugha ya matusi.



Hatua hiyo ilifikiwa leo Januari 18, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.


Upande wa Jamhuri ulidai kuwa mshtakiwa anatuhumiwa na mashtaka manne, wanadaiwa kuyatenda Julai 21,2023 eneo la Mrima Kisutu, katika jengo la Lohana Wilaya ya Ilala alimjeruhi jirani yake.

Ilidaiwa kuwa Chiku baada ya kumjeruhi mke wa jirani yake, alisababishia madhara makubwa  Kiran Lalit kwa kumzamisha kichwa chake kwenye ndoo ya saruji iliyomsababishia majeraha katika macho, masikio na kumsababishia maumivu shingoni.

Katika shitaka la pili la shambulio la mwili linalomkabili Chiku, siku ya tukio la kwanza na eneo hilo alimsababishia madhara kwa kumshambulia jirani yake Lalit Ratilal katika mwili wake kwa kumpiga ngumi na mateke kichwani.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la tatu na la nne linalomkabili Sangita, siku ya tukio  alitoa lugha ya matusi dhidi ya majirani zake, Lalit na Kiran  kitendo ambacho kilisababisha uvunjivu wa amani.

Wakili wa Serikali, Frank Michael akiomba ahirisho la kesi hiyo baada ya Hakimu Lyamuya kuwa na udhuru, Mbele ya  Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga wa mahakama aliomba tarehe nyingine ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi wawili.


"Mheshimiwa tunao mashahidi wawili na tupo tayari kuendelea, lakini tulikuwa tunaomba tarehe nyingine ya usikilizwaji kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hii hayupo," alidai Wakili Michael.

Hakimu Kiswaga alisema kesi hiyo itasikilizwa Februari  19, mwaka huu na mashahidi hao wafike siku hiyo kutoa ushahidi wao.

" Mashahidi nawataka mfike tarehe hiyo na huyo shahidi ambaye amesema  tarehe hiyo hatakuwepo atawasiliana na wakili wa serikali atatoa ushahidi wake kwa njia ya mtandao 'Video Conference' kwa sababu vifaa vipo," alisema Hakimu Kiswaga.






No comments:

Post a Comment

Pages