HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 19, 2024

TAFICO YAPONGEZWA KWA JITIHADA ZA KUINUA UCHUMI WA BLUU

Na Magrethy Katengu

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo imelipongeza Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)  kwa jitihada wanazozifanya za ukarabti  wa miundombinu ili  kusaidia kuinua Uchumi wa bluu kupitia sekta ya uvuvi.



 Pongezi hizo zimetolewa   Machi,18,2024  Jijini Dar es salaaam na  Mwenyekiti wa Kamati hiyo Deo Mwasanyika walipotembelea Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kukagua Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu ya Shirika hilo ikiwemo ujenzi wa ghala la kuzalisha  Barafu ,kiwanda cha kutengenezea vyakula vya Samaki na  ,ujenzi soko la samaki la kimataifa.

"Sisi Kamati ya Bunge tunawapongeza sanaa kwa kusimamia Maono ya Mhe Rais maana kila tulipopita   tunakutana  matokeo ya kufufua mashirika yaliyoshindikana na hapa tumebaini  namna mnavyofanya kazi kwa jitihada kubwa na mmetueleza tayari mradi wa kuzalisha   barafu umeanza kufanya kazi hongereni sanaa huku mkishughulikia ununuzi wa Meli nne na kuangalia ujenzi wa soko la kimtaifa la samaki  " amesema

Hata hivyo amewasisitiza kuhakikisha wanakamilisha miradi waliyopewa kwa wakati na kusimamia fedha zilizotengwa ziefanye kazi iliyokusudiwa na kutatua changamoto ya soko la samaki  iliyokuwa inalalamikiwa muda mrefu na wavuvi .

Awali akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kwa kamati hiyo Afisa Mkurugenzi Mtendaji TAFICO Dennis Simba amesema  wizara ya Mifugo na Uvuvi itahakikisha  miradi iliyo chini ya Program ya AFDP ya ununuzi wa meli nne za Uvuvi wa Bahari kuu, Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya uvuvi , ujenzi wa kiwanda cha kutengengeneza chakula cha samaki,Ununuzinwa samani za.ofisini na kompyuta pia ununuzi wa magari ya ofisi manne ya kusimamia mradi kutekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka mfuko wa Kimataifa wa kuendeleza kilimo(agriculture)

"Uwekezaji huu ni wa muhimu sana unakwenda   kunufaisha nchi kupitia  raslimali za uvuvi zilizopo katika ukanda wa Uchumi bahari Miliki  kwani kwa muda mrefu Taifa limekuwa halinufaiki kikamilifu na raslimali hizo hususani zilizoko baharini na hivyo sasa tunakwenda kuleta mapinduzi ya uchumi wa bluu " amesema Afisa Mkurugenzi Mkuu

Aidha  Serikali kupitia Shirika la Uvuvi TAFICO itasaidia  kuongezaka ajira na Mapato ya fedha za ndani na za kigeni kusaidia kukuza pato la Taifa pia kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza zaidi katika uvuvi,ukuzaji viumbe maji,uchakataji,pamoja na mauzo ya mazao ya uvuvi hapa nchini kwa kutumia mbinu na teknolojia ya kisasa.


No comments:

Post a Comment

Pages