Waziri
wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, ameelekeza vituo vyote vya afya, ikiwa ni
pamoja na vile vya binafsi na vya umma, vilivyosaini mikataba na Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kuendelea kutekeleza mikataba hiyo
ipasavyo.
Akizungumza na vyombo vya habari mkoani Lindi, Machi
01, 2024 Waziri Ummy amesisitiza umuhimu wa kila mtoa huduma kwa
wanachama wa NHIF kuheshimu na kufuata masharti ya mikataba waliyoingia
na NHIF. Amesema kwamba ni wajibu wa vituo vyote vya afya kutoa huduma
kulingana na makubaliano yaliyomo katika mikataba hiyo.
"Kila mtoa
huduma za afya kwa wanachama wa NHIF ameingia mkataba na NHIF, hivyo
wazingatie masharti ya mikataba walioingia na NHIF katika kuwahudumia
wanachama". Amesema Waziri Ummy
Aidha, Waziri Ummy amezitaka
hospitali zote binafsi ambazo zilikuwa zimesitisha kutoa huduma kwa
wanachama wa NHIF kuendelea kutoa huduma hizo. Amesema kamati ya
kitaalamu imeundwa kwa ajili ya kufanya majadiliano na watoa huduma
wakati huduma zikiendelea kutolewa, na kwamba majadiliano hayo
yataendelea huku huduma zikiwa bado zinaendelea kutolewa.
Aidha,
ameelekeza hospitali zote, za umma na binafsi, kuwapokea wagonjwa wa
dharura kulingana na matakwa ya sheria za usajili wa vituo vya afya na
kwamba ni kinyume cha sheria kutowapokea wagonjwa wa dharura na kwamba
hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.
"Nazielekeza
hospitali au vituo vyote binafsi na vya umma kuendelea kuwapokea
wagonjwa wa dharura pindi wanapofika katika vituo vyao kwani hili ni
takwa la kisheria namba 151 la usajili wa vituo binafsi vya afya na
kanuni yake namba 32, kutokuwapokea wagonjwa wa dharura ni kuvunja
sheria". Amesema Waziri Ummy
Hata hivyo, Waziri Ummy ametoa onyo
kali kwa watoa huduma ambao wamekuwa wakitangaza nia ya kuwaondoa
wagonjwa waliopo wodini ndani ya masaa 48. Amesema kuondoa wagonjwa hao
ni kinyume cha sheria na ni kuvunja haki za wagonjwa.
“Nimeona
habari au tangazo wakisema watawatoa wagonjwa waliopo wodini ndani ya
masaa 48 nataka kusema ni marufuku kuondoa wagonjwa waliopo wodini
kwasababu kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya madakatari". Amesema Waziri
Ummy
Pia, amezitaka hospitali za serikali,kujiandaa vyema na
kuweka utaratibu mzuri wa kupokea wagonjwa wengi zaidi ambao wanaweza
kushindwa kupata huduma katika vituo binafsi huku akisisitiza umuhimu wa
kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma bora za afya kulingana
na haki yake.
March 04, 2024
Home
Unlabelled
VITUO BINAFSI VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VYAELEKEZWA KUZINGATIA MASHARTI YA MIKATABA NA NHIF
VITUO BINAFSI VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VYAELEKEZWA KUZINGATIA MASHARTI YA MIKATABA NA NHIF
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment