HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2024

NI KISASI AMA AIBU LUPASO KESHO??

Na John Richard Marwa

Masaa you aliyobaki ni dhahiri shahiri Ngoma ipo pale kwa Mkapa. Ni Karikooo Derby, ni zaidi ya mechi ambayo Ahmed Arajiga atasimamia dakika 90 za jasho, damu na hisia kwa miamba ya Simba na Yanga kupepetana.

Ni mchezo ambao kila timu inahitaji point tatu kwa mahitaji yake. Yanga wanahitaji pointi tatu kwa Mnyama Simba ili kupanua wigo wa alama na kujihakikishia kutwaa ubigwa mara ya tatu mtawalia wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Wakati huo Mnyama Simba anahitaji point tatu za maisha yake kwenye msimu huu wa 2023/24 ambapo licha ya kutaka kurejesha furaha kwa wanasimba lakini ndiyo mechi inaweza kuwaweka imara kwenye mbio za kulisaka taji msimu huu.

Matokeo ya mchezo wa kwanza ni sababu nyingine kwa vijana wa Abderhack Benchika kutaka huo mchezo kivyovyote.

Ni nini kitatokea kwa miamba hiyo ni kusubiri kuona. Ni mchezo ambao tayali umeshachukua sura mpya na unaenda kuandika hostoria mpya katika Soka la ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara.


No comments:

Post a Comment

Pages