HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 21, 2024

TRA YAVITAKA VYAMA VYA USHIRIKA KUZINGATIA SHERIA YA KODI

Na Jasmine shamwepu, Dodoma



MAMLAKA Mapato Tanzania (TRA) imevitaka vyama vya ushirika nchini  kufuata miongozo ya uendeshaji wa vyama hivyo pamoja na kutunza nyaraka sambamba na kuhakikisha wanalipa kodi halali kwa serikali pamoja na tozo mbalimbali wanazotakiwa kulipa kama sheria ya Kodi inavyotaka.


Akizungumza Jijini Dodoma na viongozi wa vyama vya ushirika nchini Afisa Kodi TRA Mkoa wa Dodoma Daniel Kingu amesema vyama vya ushirika vina wajibu wa kulipa kodi.


Amesema vyama vya ushirika vinatakiwa kulipa kodi Kwa sababu wanajishughulisha na shughuli za kiuchumi ambazo zinawapatia kipato ambapo Kwa mujibu wa sheria za Kodi wanachaji Kodi kwenye kipato.
 




Awali Mkurugenzi wa Ushauri nanutafuti shirika la ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika COASCO GOLDEN KAJABA amesema kutokana na elimu wanayoendelea kutoa Kwa Sasa kumekuwa na mabadiliko haswa kwenye usimamizi wa mahesabu na kuzingatia sheria.

Amesema awali walikuwa wanakagua vyama elfu 6 na kukuta ni Asilimia mbili Hadi nne tu ndio wanapata hati safi na vilivyokuwa vikipata hati safi na vilivyokuwa vikipata hati isiyo na Naomi vilikuwa vingi lakini Kwa Sasa kuna  mabadiliko makubwa.



Kwa upande wao wanaushirika wameomba kuendelea kupewa elimu juu ya Kodi kwenye vyama vya ushirika kwani vingi havina ueelewa na Kodi hiyo.



No comments:

Post a Comment

Pages