HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2024

Tume ya Nguvu za Atomu yaanika mafanikio chini ya Rais Samia


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Profesa Lazaro Busagala, akizungumza na Wahariri na Waandishi wakati wa kikao kazi cha Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR) na kufanyika jijini Dar es Salaan leo Aprili 29, 2024.

Afisa Mwandamizi wa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri, akizungumza katika mkutano huo.



 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Peter Ngamilo,  akifafanua jambo wakati wa kikao kazi cha Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichoratibiwa na Ofisa ya Msajili wa Hazina (TR) jijini Dar es Salaan leo Aprili 29, 2024.

Baadhi ya Wahariri wakifuatilia mkutano huo.




NA MWANDISHI WETU

 

TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), imeanika mafanikio iliyoyapata katika miaka mitatu ya Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ikiwemo ujenzi wa Maabara na Ofisi za Kanda zenye thamani ya Sh. Bilioni 28.11, pamoja na kuongeza Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali kutoka bilioni 8.7 hadi bilioni 10.9.

Katika kipindi cha mwaka 2020/21 hadi 2022/23, Serikali imesogeza huduma kwa wananchi kwa kujenga miundombinu inayoipa TAEC uwezo wa kutoa huduma kwa jamii, ambako imejenga majengo sita ya Maabara na Ofisi za Kanda, katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya Mwanza na Zanzibar.

Kwa mujibu Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala, tume hiyo ambayo moja ya majukumu yake ni Kusimamia na Kudhibiti Matumizi Salama ya Mionzi, imetenga bajeti ya Sh. Bilioni 10.47 kufanikisha ujenzi wa Maabara na Ofisi za Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha.

Akizungumza na wanahabari, Prof Busagala alisema kuwa gharama za Maabara na Ofisi za Kanda za TAEC, ambayo pia ina jukumu la Kuhamasisha na Kuendeleza Matumizi Salama ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia nchini, ni; Kanda ya Mashariki Dar (Sh. Bilioni 7.91) na Makao Makuu Dodoma (Sh. Bilioni 3.84).

“Pia, imetengwa bajeti ya Sh. Bilioni 3.03 za ujenzi wa Maabara na Ofisi za Kanda ya Zanzibar na Sh. Bilioni 2.85 kwa ajili ya Kanda ya Ziwa jijini Mwanza, majengo manne kati ya hayo sita kwenye kanda tano, yameshakamilika, na hii sasa inafanya jumla ya Ofisi za TAEC kufikia 63 Bara na Visiwani.

“Katika Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali, yameongezeka kutoka bilioni 8.7 Mwaka wa Fedha wa 2020/2021 hadi kufikia bilioni 10.9 Mwaka wa Fedha wa 2022/2023, siri ya mafanikio hay ani juhudi za Serikali ya Rais Samia kufungua Ofisi za Kanda na Mipakani na kutumia Mifumo ya TEHAMA.

“Hapa naizungumzia TEHAMA ambayo Serikali imeboresha matumizi yake, maboresho yaliyosaidia sana kufanikisha utekelezaji wa majukumu na ufanisi katika kuunganisha Mifumo ya TAEC (EDMS)ili ifanye kazi kwa pamoja na mifumo mingine ya Serikali kama vile GePG, TANCIS, TeSWS, iliyochangia matokeo chanya ya TAEC.

“Aidha, Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TAEC, iko katika hatua za mwisho kukamilisha mpango wa ufadhili kwa vijana wa Kitanzania kusoma vyuo vya nje ya nchi masomo ya Teknolojia na Sayansi ya Nyuklia katika ngazi ya Shahada za Uzamili,” alibainisha Prof. Busagala katika taarifa hiyo.

Aliongeza ya kwamba, kila mwaka vijana watano wa Kitanzania watapata ufadhili huo wenye lengo la kuongeza idadi ya wataalamu wa Nyanja ya Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia ili kuhakikisha kwamba taifa linanufaika ipasavyo na Fursa za Sayansi ya Nyuklia.

Katika uboreshaji wa Tafiti za Teknolojia ya Nyuklia, Prof. Busagala alibainisha ya kwamba Serikali imeongeza tengeo la Bajeti ya Utafiti TAEC hadi kufikia Sh. Milioni 450 katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, juhudi zote zikilenga kupata fursa zaidi za Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia na kuwalinda wananchi na madhara ya mionzi.

Mafanikio ya TAEC katika miaka mitatu ya Rais Samia yamegawanyika katika maeneo mbalimbali, yakiwemo; Kuongezeka kwa Usimamizi wa Matumizi ya Mionzi na Teknolojia ya Nyuklia, Ununuzi wa Vifaa vya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia na Kuboresha Tafiti za Teknolojia ya Nyuklia

No comments:

Post a Comment

Pages