HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 23, 2024

Yashauriwa kutengwa bajeti ya vitabu vya kiada

Na Mwandishi Wetu


Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Dk John Kalaghe ameshauri kutengwa kwa bajeti maalum kwa ajili ya uchapaji na usambazaji wa vitabu vya kiada mashuleni kwa kuzingatia kuwa vitabu hivyo ni vipya.

Aidha kuweka mpango maalum wa usambazaji wa vitabu hivyo mashuleni ikiainishwa muda mahususi wa ukamilishaji wa zoezi hilo.

Amesema mpango huo utasaidia shule, walimu na jamii kujipanga na kuchangia katika maeneo ambayo serikali itachelewa kuyafikia.

Awali amesema pamoja na kazi kubwa ambayo serikali imefanya hasa katika utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa na uandaaji wa vitabu vya kinda kwa wanafunzi wa elimu ya awali na msingi,

Uchambuzi uliofamywa na HakiElimu unaonesha shule nyingi hasa za umma bado hazijapata nakala ngumu ya vitabu hivyo kwa ajili ya utekelezaji.

No comments:

Post a Comment

Pages