Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa pili kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Orbit Security Co. Ltd, Godfrey Gabriel, wakibadilishana Nyaraka baada ya kusainiana mkataba wa benki ya NMB kuwa Wakala wa Madalali wa Soko la Hisa na wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE, Mary Mniwasa na (kushoto) ni Mhazini Mkuu wa NMB Aziz Chacha.
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya NMB imepata idhini kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya
Soko la Mitaji na Dhamana (CSMA) kuwa wakala wa madalali wa Soko la Hisa
Dar es Salaam (DSE).
Kupitia
idhini hiyo wananchi sasa wataweza kuuza na kununua hisa na hatifungani
kupitia mtandao mpana wa matawi 231 wa Benki ya NMB yaliyopo nchi
nzima.
Akizungumza
wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Mawasiliano baina (MoU)
baina ya Benki ya NMB na kampuni ya dalali wa hisa ya Orbit Securities,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna huku akiinukuu ripoti
ya Finscope ya mwaka 2023 alisema asilimia 0.5 tu ya waTanzania
wanatumia soko la mitaji kuwekeza.
“Nina
imani kwamba makubaliano haya ya kimkakati yatafungua ukurasa mpya siyo
tu kwa Kampuniu ya Orbit Securities bali na madalali wengine wa Soko la
Hisa la Dar es Salaam. Natumia nafasi hii kuwakaribidsha madalali
wengine kuja kuingia makubaliano nasi ilikuwawezesha waTanzania wengi
zaidi kutumia masoko ya mitaji,” alisema.
Alitoa
shukrani kwa Benki Kuu ya Tanzania na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na
Dhamana (CMSA) kwa kutoa idhini kwa benki yake huku akisistiza kuwa
hatua hiyo inaonyesha imani kubwa kwa benki yake.
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Orbit Securities Godfrey Gabriel
wakati wa hafla hiyo alisema, “Hii ni siku muhimu na ushirikiano huu
utafungua milango kwa watu binafsi na wafanyabiashara kushiriki katika
masoko ya mitaji kwa urahisi zaidi,”
Gabriel
aliongeza kuwa makubaliano haya yanalenga kuunga mkono mpango wa
maendeleo ya sekta ya fedha pamoja na sekta ya mitaji na dhamana
ilikufanikisha lengo la ujumuishaji wa kifadha unaolenga kuongeza
ushiriki wa waTanzania katika soko la mitaji na dhamana kufikia asilimia
5.
“Makubaliano
yetu na Benki ya NMB yatarahisisha fursa za uwekezaji. Tunatoa shukrani
kwa Benki Kuu ya Tanzania kwa kutoa idhini ya ushirikiano huu na Benki
ya NMB,” alisema.
Naye
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Mary
Mniwasa katika hafla hiyo alisema, “Siku ya leo ni siku muhimu na
yakipekee katika soko la mitaji. Kwa kweli, hatua kama hii tumekuwa
tukisubiri kwa miaka mingi sana ukweli madalali wetu wengi bado ni
wadogo na hawana mtandao mkubwa,”
Mniwasa
alisema kupitia ushirikiano huo mpya wa Benki ya NMB na Kampuni ya
Orbit Securities, soko la hisa sasa litafikiwa kuirahisi zaid kupitia
mtandao mpana wa Benki ya NMB.
“Natoa
pongezi kwa uongozi wa Benki ya NMB pamoja na kampuni ya Orbit
Securities kwa kufungua ukrasa mpya wa ushirikiano. Ni matumini yangu
kuwa ushirikano huu utaongeza uwekezaji wa tija katika Soko la Hisa la
Dar es Salaam,”
Aidha
Mniwasa aliipongeza Benki ya NMB kwa uthubutu wake wa kuorodhesha kwa
hatifungani yake ya Jamii Bond katika Soko la Hisa la London (LSE) siku
chache zilizopita.
“Kwa
kuorodhesha hati fungani katika masoko makubwa kama Soko la Hisa ya
London na Soko la Hisa la Luxemberg, NMB inaendelea kupeperusha bendera
ya nchi yetu vyema,” alisema.
No comments:
Post a Comment