HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 01, 2024

KIBAHA DC KUNOGILE MWENGE WA UHURU WATOA BARAKA KWA MIRADI YOTE 13 YA MAENDELEO

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA 

Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imeweza kupata baraka baada ya kiongozi wa  mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Msava kuridhishwa na kupitisha miradi yote 13 ya mandeleo.
Kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa amepitisha miradi yote  hiyo 13 ambayo  imepitiwa na mwenge wa uhuru na kuwapongeza viongozi mbali mbali ambao wameweza kuhakikisha wanaisimamia vema na kutumia fedha vizuri ambazo zimetolewa  na serikali kwa kuzingatia mfumo wa kidigitali.

Alisema kwamba licha ya kuridhishwa na miradi hiyo mbali mbali ya maendeleo lakini ameagiza baadhi ya miradi ambayo imeonekana kuna na dosari  kadhaa wahakikishe wanazifanyia kazi na kuzirekebisha.

"Nawapongeza viongozi wote wa halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwa kuweza kutekeleza miradi yenu kwa vitendo na kitu kikubwa fedha ambazo zinatolewa na serikali zitumike vizuri katika kutekeleza miradi ya maendeleo "alisema Mzava

Kadhalika aliongeza kuwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan anatenga fedha kwa ajili ya miradi mbali mbali ili kuwasogezea huduma wananchi hivyo viongozi na watendaji wanapaswa kusimamia miradi hiyo kwa maslahi ya wananchi.

Mwenge wa uhuru umepita katika miradi mbali mbali ya maendeleo ambapo umekagua mradi mkubwa wa kongani ya viwanda 
ya  SINOTAN, uliopo Kata ya Kwala ambao  utagharimu kiasi cha shilingi  trilioni 8.4. mpaka kukamilika kwake.

Pia Mwenge huo wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika  mradi wa ujenzi wa barabara kutoka barabara ya Morogoro kwenda ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yenye urefu wa mita  zipatazo 300  ikiwa katika kiwango cha lami.

Aidha mwenge wa uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha pia umepitia miradi mingine ya maendeleo ikiwemo uzinduzi wa  zahanati ya Vikuruti ambayo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Kadhali iliweza kuzindua mradi mkubwa wa maji ambao unatekelezwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira(RUWASA) ambao umegharimu kiasi cha shilingi 328.

Sambamba na hilo mbio za Mwenge wa uhuru umeweza kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika sekta mbali mbali ikiwemo,afya,elimu,maji miundombinu ya barabara mapambano ya rushwa ukimwi,lishe pamoja na miradi mingine ya maendeleo.

Awali akiupokea Mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon alibainisha kwamba Mwenge huo katika Halmashauri mbili za Kibaha mji na Wilaya ya Kibaha utazindua jumla ya miradi 28 yenye thamani ya shilingi trilioni 8.5.

Nao baadhi ya wananchi ambao waliweza kupata fursa ya kushiriki katika mbio hizo wameshukuru Mwenge wa uhuru kwa kuweza kuzindua baadhi ya miradi na mingine kuweka mawe ya msingi ambayo kwa upande wao ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia huduma muhimu za kijamii.

No comments:

Post a Comment

Pages