NA VICTOR MASANGU, DAR
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka wa 2024 Godfrey Msava
amewapongeza kwa dhati viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza
kuwa kitu kimoja katika kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo
imempelekea kuridhishwa na kuipitisha miradi 26 kati ya 28
iliyotembelewa.
Kiongozi
huyo alibainisha kwamba amefurahishwa kuona ushirikiano mzuri alionao
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge pamoja na timu yake nzima ya
wakuu wa Wilaya,wakurugenzi pamoja viongozi wengine kwa kuwapa
ushirikiano katika kipindi chote walipokuwa katika kutembelea miradi
mbali mbali.
"Tumetembelea miradi mbali mbali ya maendeleo katika
Mkoa wa Pwani na nimefarijika kuona idadi kubwa tumeweza kuifungua na
mingine kuiwekea mawe ya msingi lengo kubwa ni wananchi wetu waweze
kupata huduma stahiki kwani Rais wetu anatoa fedha kwa ajili
hiyo,"alisema Mzava.
Mzava aliyabainisha hayo leo wakati wa
halfa fupi ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru ambao ulikuwa unatokea
Wilayani Mafia na kukabidhiwa rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Albert Chalamila.
"Nawashukuru sana kwa dhati viongozi wote
wa Mkoa wa Pwani kwa kututunza tangu siku ya kwanza hadi hii leo hatuna
budi kuondoka lakini kiukweli mmefanya kazi kubwa katika miradi yenu kwa
hiyo niwapongeze sana Mkuu wa Mkoa na timu yako yote,"alisema Mzava.
Pia
alisema katika Mkoa wa Pwani tangu wapokelewa wameweza kupata fursa ya
kutembelea,kugagua na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo
imeweza kugusa katika nyanja mbali mbali.
Pia aliwaomba
viongozi kuendelea kusimamia fedha ambazo zinatolewa na Rais wa awamu ya
sita na katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuwakumbusha kuifanyia
kazi miradi ambayo imeonekana kuwa na dosari.
Awali Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akisoma taarifa kwa kiongozi huyo
alibainisha kwamba mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa zimeweza kukimbizwa
katika Halmashauri tisa zilizopo katika Wilaya saba za Mkoa wa Pwani.
Kunenge
alibainishwa kwamba katika Mbio hizo zimeweza kupita katika miradi 28
ambayo kati ya hiyo miradi 26 ya maendeleo imeweza kupitishwa na miradi
miwili haikuweza kupitishwa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya dosari
katika miradi miwili ambayo nayo itasimamiwa na kufanyiwa kazi.
Kadhalika
Kunenge alifafanua kwamba miradi yote ambayo imepitiwa na mbio za
Mwenge wa uhuru ina jumla ya thamani ya kiasi cha shilingi trilioni 8.5.
Pia Kunenge alimpongezs Rais wa awamu ya sita Dkt..
Samia
Suluhu Hassan kwa kuweza kutafuta fedha mbali mbali pamoja na
kushirikisha wadau kwa lengo la kuweza kuwaletea wananchi maendeleo.
Mbio
za Mwenge wa uhuru kitaifa ukiwa katika Mkoa wa Pwani umeweza
kukagua,kuzindua,kuweka mawe ya msingi pamoja na kupitia miradi mbali
mbali za maendeleo ikiwemo afya,elimu,
maji,barabara,rushwa,ukimwi,madawa ya kulevya,shughuli za kimaendeleo na
mambo mengine ya kijamii.
No comments:
Post a Comment