HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2024

Wanahisa CRDB wapitisha gawio la hisa moja Sh. 50, Siri ya Mafanikio yatajwa


 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB jijini Arusha leo Mei 18, 2024.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB uliofanyika jijini Arusha leo Mei 18, 2024.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakarugenzi Benki ya CRDB, Dk. Ally Laay, akizungumza wamati wa mkutano wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugezi wa Benki ya CRDB Prof. Neema Mori, akitoa hotuba yake wakati akifunga Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB jijini Arusha.

 Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, akiwasilisha taarifa ya fedha katika Mkutano Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB. 




Mshiriki wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB akijisajili kidijitali.

 

 
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

  

MKUTANO Mkuu wa 29 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, umefanyika Jumamosi ya Mei 18 jijini Arusha, ambako Wanahisa wameidhinisha gawio la Sh. 50 kwa hisa moja, huku Mkurugenzi Mtendaji Abdulmajid Nsekela akifichua siri ya mafanikio yao kuwa ni pamoja na ufanisi kiutendaji, kujitanua kibiashara ndani na nje ya nchi, pamoja na Uwekezaji wa Huduma za Kidijitali.

Mkutano wa Wanahisa wa CRDB ulifunguliwa Ijumaa Mei 17 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye alikiri kuvutiwa na mafanikio ya mwaka wa kwanza kati ya mitano ya Mkakati wa Biashara wa Muda wa Kati wa mwaka 2023-2027 ambako benki hiyo ilivuna faida baada ya Kodi ya Sh. Bilioni 424.

Akizungumza na wanahabari baada ya kufunga mkutano huo, Nsekela aliwashukuru Wanahisa wa CRDB kwa kushiriki, kutoa mapendekezo sahihi ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya benki hiyo, lakini zaidi kwa kupitisha gawio la shilingi 50 kwa kila hisa.

"Ni mkutano muhimu sana kiajenda, kwani umetumika kukusanya maoni ya Wanahisa kuelekea mwaka ujao wa fedha, ambako wametoa mapendekezo chanya yatakayochagiza ukuaji wa faida na pato la benki kwa ujumla wake, lakini zaidi wamepitisha gawio rekodi la shilingi 50 kwa hisa moja.

"Tumeutumia mkutano huu kuwaeleza siri za mafanikio ya benki yetu, ambazo ni pamoja na ufanisi kiutendaji, kujitanua ndani na nje ya nchi, ambako tumefungua matawi na Kampuni washirika nchini Burundi na Congo DR, Uwekezaji katika utoaji huduma Kidijitali na maeneo mengineyo mengi.

"Kama haitoshi, CRDB tumejikita katika kuisapoti Serikali Sekta za Kimkakati ikiwemo Utalii, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, pamoja na kupunguza mikopo chechefu hadi kufikia asilimia 2.9 kwa kuwafanyia chambuzi yakinifu wakopaji wetu na kuondoa viatarishi kwa ongezeko la aina hiyo ya mikopo.

"Haya yote yamekuwa chachu ya mafanikio yetu, kwani ukiondoa faida baada ya Kodi ya Sh. Bilioni 424 tuliyopata mwaka Jana, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza kati ya mitano ya Mkakati wa Biashara wa Muda wa Kati wa Mwaka 2023-2027, dalili za kuvunja rekodi zinaonekana, kwani tumeandikisha rekodi ya Sh. 128 katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2024," alisema Nsekela.

Aidha, Nsekela alibainisha ya gawio la wanahisa linaongezeka na kukua mwaka baada ya mwaka, mafanikio ambayo yamechochewa na sera nzuri na Mazingira Wezeshi yaliyowekwa na Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye wamejipanga kumsapoti vema katika mkakati wake wa Nishati Safi ya Kupikia, ambako waliungana naye katika Mkutano wa kujadili hilo nchini Ufaransa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Dk. Ally Hussein Laay, alitambia mafanikio makubwa ya benki yake yaliyoongeza gawio la wanahisa na kwamba kwa aina ya Uwekezaji walioufanya ndani na nje ya nchi, Wana matumaini makubwa ya kuongezeka kwa faida baada ya kodi kuanzia mwaka huu na kukua kwa gawio la wanahisa.

"Tumefanya Uwekezaji mkubwa sana katika mtandao wa matawi na huduma, tumeanzisha Kampuni Tanzu kadhaa nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokeasia ya Congo (DRC), na kuanzia mwakani faida ya benki na gawio vitavunja rekodi.

"Mikopo chechefu imepungua na hii ni kutokana na ufanisi katika kuchambua taarifa za kifedha za wakopaji wetu. Miaka minne au mitano iliyopita, kiwango cha mikopo chechefu nilikuwa asilimia 13, lakini Sasa tunaizingumzia CRDB ambayo mikopo chechefu iko chini ya asilimia tatu," alisema Dk. Laay.

Aidha, Dk. Laay alisema Bodi ya Wakurugenzi imetengeneza Mkakati wa Biashara wa Muda wa Kati wa mwaka 2023-2027 na kwamba waendako mtandao wa matawi ya benki hiyo utatanuka zaidi, ambako watafungua matawi nchini Zambia, Dubai na Comoro, ambako wanaamini kutachochea mafanikio na faida kubwa zaidi.
 

No comments:

Post a Comment

Pages