HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 14, 2024

SERIKALI YAJIDHATITI UDANGANYIFU WA SHAHADA HEWA VYUO VIKUU

Na Mwandishi Wetu

Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mamlaka ya Vyuo vikuu Tanzania (TCU) wamejidhatiti kulinda heshima ya mfumo wa eiimu nchini kwa maslahi mapana ya Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kuwepo kwa taarifa na tuhuma za udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya Vyuo Vikuu nchini.

"Hapa karibuni kumekuwa na tuhuma zinaeleza rushwa kutoka kwa vyombo vya habari kwamba kuna udanganyifu kwenye vyuo vikuu hasa katika masuala ya mitihani na tuhuma hizo zimerudiwa  mara kadhaa na sisi kila tuhuma tukizipata tunazifanyia kazi na tuna omba mtu yoyote ambaye anahisi kuna suala analifahamu alilete TCU moja kwa moja litafanyiwa kazi.

Lakini tuona sasa tuhuma hizi zinavyosemwa zinaweza zikasababisha watu wakadhani kwamba hali ya vyuo vikuu vyetu ni mbaya sana, napenda kuwahakikishia watanzania wote kwamba bado vyuo vikuu vyetu vikuu vinazingatia sana maadili hasa katika masuala ya mitihani na weledi kuhakikisha kwamba tunatoa shahada kwa mujibu wa taratibu zinazokubarika katika taaluma zetu."amesema Mkenda na kuongeza kuwa.

"Suala la udanganyifu majaribio ya udanganyifu yapo Dunia nzima na kwa nchi zote mahali popote Duniani suala kubwa ni juhudi ambazo zinatumika kuzuia udanganyifu na kila tunaposikia tuhuma tunachukulia ni jambo zito sana na ntawakumbusha tu kulikuwa na dalili kama hizo kwa mitihani ya darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita na mitihani inayosimamwiwa na Baraza la mitihani tulianza kuchukua hatua na tulichukua hatua kali ambazo kwa bahati mbaya zinaumiza hata masilahi ya baadhi ya wawekezaji wa elimu kwaiyo tulizichukua pamoja na mashinikizo ambayo wakati mwingine unayapata na lawama chungu nzima lakini tulisimama imara kwa sababu ya udanganyifu wa mitihani madhara yake ni makubwa sana, kwanza kabisa ni suala ambalo linaondoa usawa, tunataka wanafunzi wanapofanya mitihani wote wapimwe kwa usawa na haki, mmoja asiwe anadanganya anapita na mwingine anatumia juhudi zake anapita.

"Hili ni suala la weledi, unapokuwa umeondoa weledi kwamba mtu mwingine anaweza akapata cheti kwa sababu ya udanganyifu halafu anaweza akapewa majukumu ya kwenda kuhudumia umma, tuseme labda amesomea udaktari lakini akafanya udanganyifu halafu ataenda kutibu mtu madhara yake ni makubwa sana kwa wale ambao wanapata huduma hiyo.

"Na vilevile tukirushusu udanganyifu kwenye elimu ni kama vile kulea ama kuruhusu rushwa kwa wanafunzi wetu kwamba wewe mwanafunzi njia nzuri ya kuendelea ni kuwa mdangaanyifu na ndio maana hatua ambazo tumezichukua baadhi ya watu wanalaumu kwamba tumekuwa wakali sana na naomba tu umma utuelewe kwamba tunafanya hivyo kwa kulinda heshima ya mfumo wetu wa elimu kwaiyo mliona kwenye Baraza la mitihani tumesimama kidete hasa tumeleta mabadiliko ya sheria ili kuwabana zaidi wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani." amesema Mkenda na kubainisha kuwa.

"Sasa kuhusu vyuo vikuu, vyuo vikuu vyote vina kanuni za kusimamia mitihani ambazo zinafahamika na TCU na kwa kawaida Chuo Kikuu ukikamatwa umedanganya kwenye mtihani adhabu yake ni kufukuzwa Chuo moja kwa moja, ukishapata uhakika kwamba umedanganya mtihani hukumu yake unafukuzwa chuoni.

"Mimi nina watu chungu nzima ofisini wazazi wao wanaomba kwa waziri, tunaomba mwanetu arudi alifukuzwa, ameonewa, ninachofanya nikurudi kwenye utaratibu wa Chuo kuuliza nini kimetokea, unakuta utaratibu ulifanyika Baraza limemfukuza Chuo amepewa muda wa kukata rufaa hajakata ama amekata lakini mimi kama waziri nimekataa kata kata kuingilia mamlaka ya vyuo vikuu wanapochukua hatua kama hizo kwa sababu tunalinda sana suala la mitihani.

"Sasa tuhuma zingine ni kwamba ambazo tumeziona zimetoka kwenye gazeti moja kwamba kuna utaratibu wa wanafunzi kuhonga ili matokeo yaliyokwisha ingizwa kwenye mfumo wa tehama yabadilishwe, sasa kulitokea tuhuma kama hizo katika chuo kimoja hapa nchini na kikamtaja jina la mwanafunzi na mtu ambaye alihusika kubadilisha yale matokeo, nilimwambia Katibu Mkuu aunde tume huru kwenda kuchunguza, ikiwa ni pamoja na idara ya usalama wa Taifa na wataalamu wa tehama, waliingia wakaangalia mfumo wote wa tehama uzuri ukishaingiza matokeo yote kwenye tehema mabadiliko yeyote yanayofanyika yanaacha kumbukumbu ya mabadiliko, lazima utaona mtu aliingia saa ngapi aliingiza alama ngapi nautaona tarehe ngapi hizo alama zilibadilishwa.

"Kwaiyo tulichunguza tukagundua si kweli na kwenye Chuo hicho nadhani kuna mnyukano tu, kuna mtu au watu kwa sababu wanajua makamu Mkuu wa Chuo anastaafu karibuni basi sijui ni kuchafuana huko kwa sababu kuna dalili kwamba katika kinyang'anyiro cha kutaka kuchukua nafasi watu wanachafuana lakini nasema hivi Katibu Mkuu tumekubalina ataiomba TCRA ichukue Chuo kilekile kama majaribio kwa sababu ya tuhuma tulizozisoma kwenye gazeti kwenda kufanya uchunguzi wa matokeo yote ambayo yameingizwa kwenye  tehama na kuangalia matokeo yanapoingizwa yanapobadilika nani anabadilisha.

Pamoja na hayo Waziri Mkenda amewaomba waandishi wa Habari kutoa ushirikiona pale unapohitajika juu taarifa wanazoziandika ili kuweza kulisaidia Taifa na sekta ya elimu juu udanganyifu unaofanyika katika mitihani na vyuo vinavyohusika.

Vile amesema wataendelea kuchukua hatua kali kwa maslahi mapana ya mfumo mzima wa elimu na wataalamu wanaozalishwa nchini kupitia Vyuo Vikuu nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages