HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 07, 2022

FUATA TARATIBU ZA KUFUNGA BIASHARA YAKO KUEPUKA HAYA


Afisa Huduma TRA Mkoa wa Kagera,
Alex Mwambenja.

 

Na Lydia Lugakila

Wafanyabiashara Mkoani Kagera wametakiwa kufuata taratibu za kufunga biashara ili kuepuka kudaiwa kodi za vipindi vilivyobakia katika mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Alex Mwambenja ambaye ni Afisa huduma TRA  mkoa wa Kagera akikazia juu ya tangazo la kitaifa

Bwana Alex amesema kuwa wafanyabiashara wanapotaka kufunga biashara wanatakiwa kufuata  taratibu za kufunga biashara zao ikiwa ni pamoja na kupeleka barua TRA juu ya kufunga biashara hiyo na kuhakikisha imethibitishwa na serikali ya mtaa husika.

Aidha katika hatua nyingine Mwambenja amesema kuwa mfanya biashara atatakiwa kuhakikisha anarejesha cheti cha TIN cha biashara katika ofisi ya TRA na  kuwa kwa kufanya hivyo kutamsaidia mfanyabiashara kutodaiwa kodi za vipindi vilivyobakia katika mwaka.

No comments:

Post a Comment

Pages