HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 06, 2024

400 KUFANYIWA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO

 Na WAF – Songwe

Watu zaidi ya 400, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho mkoani Songwe na maeneo jirani ikiwa ni jitihada za Serikali kusogeza huduma za kibingwa na Ubingwa Bobezi karibu na wananchi.

Huduma hiyo itakayotolewa Bure kwa muda wa Siku tano imeratibiwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Kushirikiana na Shirika la Hellen Keller.

 

Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Songwe Dkt. Ntufye Kapesa Agasti 5, 2024 wakati wa siku ya kwanza ya  kambi ya huduma za matibabu ya upasuaji wa mtoto wa jicho katika Hospitali ya wilaya hiyo.

Wagonjwa wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wametoka katika kata zote kumi na nane za Wilaya ya Songwe ambapo itadumu hadi Agosti 09,2024" amesema Dkt. Kapesa
 
Wagonjwa waliofuatwa kwenye kata zao kwa kutumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii  na usafiri bure, pia wanapokuwa hapa wao na ndugu zao watahudumiwa chakula bure na kurudishwa makwao, pia mpango huo utasaidia kuitangaza hospitali ya wiliya ya songwe kwani  hospitali bado ni mpya” amesisiti Kapesa.
 
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Songwe, Godfrey Kawacha amesema jamii inafaidika na kufarijika kwa kupata huduma hiyo adimu kwa kuwa imewarahisishia kupata matibabu hayo kwa urahisi na bila gharama yoyote.
 
Bi. Pistina katumbi, Mkazi wa Kijiji cha mbagala mbuyuni, Wilaya yaSongwe, mkoa wa Songwe amesema amekuwa akisumbuliwa na hali ya kuto kuona kwa jicho lake moja kwa muda wa mwaka mmoja lakini kupitia kambi hiyo ameweza kufanyiwa matibabu bila gharama yoyote huku  akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu .

Awali Mganga mfawishi mbali yakuelezea kambi itakavyokuwa ameishukuru serikali kwa kuendelea kutafuta wadau mbalimbali ili kuweza kutoa huduma za matibabu ya kibingwa wa watanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages