HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila aipongeza Benki ya NMB kwa kusaidia ustawi wa walimu

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (wa pili kulia) akisalimiana na meneja Mahusiano wa Benki ya NMB na Serikali wa kanda ya Dar es Salaam, Melinda Kamukara (wapili kushoto) wakati wa kuagana na walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam waliojitokeza kupongeza utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukamilisha mradi mkubwa wa treni ya umeme ya SGR. walimu hao wamesafiri kwa treni ya SGR hadi Morogoro kiutalii kutembelea Hifadhi ya Taifa Mikumi. Kulia na afisa Mahusiano wa Benki ya NMB, Cuthbert Zimbwe na kushoto ni katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Dkt. Toba Nguvila. Benki ya NMB imetoa zaidi ya shilingi milioni 20 kusaidia ziara hiyo ya walimu.

 

Na Mwandishi Wetu

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza Benki ya NMB kwa jitihada zake za kuendelea kusaidia ustawi wa walimu nchini.

 

Chalamila alitoa pongezi hizo jana wakati wa hafla ya kuwaaga walimu 1000 walioanza ziara ya siku mbili iliyopewa jina la SGR-Mikumi jijini Dar es Salaam jana.

 

Ziara hiyo ilifadhiliwa na Benki ya NMB ambapo benki hilo ilitoa jumla ya shilingi milioni 22 ambapo milioni 12 zilighramia kuchapa fulana na shilingi milioni 10 kwa ajili ya mambo mengine.

 

"Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo zinazoanzishwa na Serikali. Nachukua fursa hii pia kuipongeza benki hii kwa kuunga mkono ziara hii ya waalimu," Chalamila alisema.

 

Aliongeza, "Walimu ni kundi la kwanza kufanya ziara ya mradi wa reli ya SGR baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan Alhamisi wiki hii. Ninaamini kuwa ziara hii sio tu itaongeza maarifa na uzoefu kwa walimu bali itakuwa chachu ya kampeni ya ‘Royal Tour’," alisisitiza.

 

Chalamila alibainisha kuwa katika mkakati wa muda mrefu wa kutangaza mradi wa reli ya SGR, ofisi yake imeandaa kuratibu ziara nyingine tarehe 30 Agosti mwaka huu ambayo itakutanisha vikundi maalum.

 

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk.Toba Nguvila wakati wa hafla hiyo alisema ziara hiyo itawapa walimu fursa ya kujifunza kwa vitendo badala ya kujifunza na kusoma kwa nadharia na kujionea ekolojoa nzima ya hifadhi ya Mikumi

 

"Hakika hii ni ziara yenye tija na ufanisi mkubwa. Tunaamini itasaidia sio tu katika kuwaongezea ari ya kazi lakini pia kuhakikisha kuwa wanakuwa mabalozi wazuri wa mradi mkubwa wa reli wa SGR unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita" alisisitiza.

 

Awali, Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Cuthbert Zimbwe wakati wa hafla hiyo alisema uhusiano wa benki hiyo na walimu una historia ndefu huku akisisitiza dhamira ya benki hiyo kuendelea kutoa bidhaa na huduma zinazokidhi matakwa ya walimu.

 

"Tumekuwa na uhusiano mzuri na walimu kwa miaka mingi sasa. Ama kwa hakika, benki yetu ina historia ndefu na walimu. Tunaamini mchango wetu katika ziara hii ya mradi wa SGR utasaidia kuweka tabasamu kwenye nyuso za waalimu.” Zimbwe alisema.

 

MWISO

No comments:

Post a Comment

Pages