HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2024

DC Mpogolo: Serikali kutatua kero za wananchi Ilala

 Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk, Samia Suluhu Hassan imedhamiria kutatua kero za wananchi wake ili kuwaletea maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akizingumza na wananchi kata nne za wilaya ya Ilala ambazo ni Pugu Stesheni,Ukonga, Kitunda na Kivule wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha Kitunda katika kata hiyo.

“Nina utaratibu wakusikiliza Mwananchi mmoja mmoja kila Alhamisi, leo nimeona nije kuwasikiliza wananchi wa kata hizi nne kwa pamoja nakuzipatia ufumbuzi kero zenu, kwani ni dhamira ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya CCM unatatua kero za wananchi” amesema Mpogolo.

Awali Mpogolo aliendesha Kikao cha ndani cha CCM na baadaye kufuatiwa na mkutano wa hadhara uliyokusanya mamia ya wakazi wa kata tajwa hapo juu nakusikiliza kero zao ambazo ni ubovu wa barabara za kata hizo ikiwemo ambap amesema serikali imejipanga kikamilifu kuanza ujenzi wa barabara katika Kata za Kivule, Mzinga, Kipunguni na Kitunda, kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP) ambao unatarajia kuanza muda wowote kuanzia sasa kwakuwa miradi hiyo imekwisha sainiwa kwa ajili ya utekelezaji wake.

 “Mwanzo tulipanga kujenga barabara zenye jumla ya urefu wa kilometa 46 lakini tumeongeza idadi ya barabara hivyo jumla ni kilometa 57  ndiyo zitakazo jengwa,” amesema Mpogogolo.

Ametaja miongoni mwa baraba zitakazo jengwa ni Kitunda- Kivule  hadi Msongola yenye urefu wa Kilmetea 9.95, Kivule -Majohe Kilomita2.79.

Kero nyingine zilizoibuliwa katika hadhara hiyo ujenzi wa kiholela, michango mingi ya shule za msingi za serikali, kukosekana kwa stendi na Tasafu kuwaondoa baadhi ya wanufaika katika orodha ya wanufaika ilihali bado wana uhitaji wa matunzo kutoka kwa Taasisi hiyo.

Kuhusu michango ya Tuisheni na mitihani isiyo na tija Mpogolo amepiga marufuku, kuhusu kaya maskini suala hilo amewachia watu wa ustawi wa jamii kufuatilia na kuahidi kwamba kwa yeyoyote mwennye dukuduku milango ya ofisi yake ipo wazi.

Lakini pia katika ziara hiyo ameambatana na wataalamu mbalimbali kwa ajili ya utatuzi wa kero za wananchi wakiwemo Tarura, Tanesco na wanasheria.

No comments:

Post a Comment

Pages