HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 13, 2024

Marekani na India Zaungana Kuendeleza Nishati Mbadala nchini Tanzania

Dar es Salaam – Septemba 12, 2024 - Serikali ya Marekani imeandaa tafrija fupi kuaga wajumbe kutoka Tanzania wanaosafiri kuelekea India kwa ajili ya programu maalum ya mafunzo ya uendeshaji wa gridi, ambayo ni hatua muhimu katika mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Marekani-India-Tanzania (TRIDEP) unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

 

Ushirikiano huu umekua tangia mwanzoni wa mwaka 2022, maafisa wakuu kutoka Tanzania walipotembelea India kupitia programu iliyowezeshwa na Serikali ya Marekani. Shirika la USAID nchini Tanzania na India limefanya kazi kwa karibu kuimarisha uhusiano kati ya serikali ya Tanzania na India kubadilishana utaalamu na kuimarisha sekta zao za nishati. Hatua hii iliendeleza ushirikiano wa TRIDEP kwa hatua moja mbele na kutangazwa rasmi mpango huu wa ushirikiano katika nishati mbadala July 2024.

 

“Nimefurahi kuona washirika wetu wa Tanzania wakianza ziara hii nchini India. Ushiriki wao katika mpango huu wa kubadilishana mafunzo unaashiria hatua kubwa ya kusonga mbele katika kuimarisha miundombinu ya nishati ya Tanzania na kuendeleza mipango ya nishati mbadala,” alisema Balozi wa Marekani nchini Dkt. Michael C. Battle. “Kuendeleza ushirikiano huu kati ya India na Tanzania ni dhamira ya serikali ya Marekani ya kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na ushirikiano unaochochea maendeleo endelevu na usalama wa nishati.”

 

Katika kipindi hiki cha kujenga uwezo kuanzia September 14 hadi 28, wajumbe kutoka Tanzania wataungana na wataalamu kutoka India na kujifunza mbinu za kisasa. Mpango huo utawapa wajumbe hao uelewa mpana wa mfumo wa umeme wa India na utendaji wake ikijumuisha sera na mifumo ya udhibiti, ujumuishaji wa nishati mbadala, na nchi za jirani, viwango vya gridi, mawasiliano na uchanganuzi.

 

“Ninafurahi kusikia maafisa wa Tanzania watatembelea Shirika la India Grid Controller kwa wiki mbili kwa ajili ya mafunzo na kujenga uwezo. Ziara hii inaonesha ushirikiano mkubwa kati ya India na Tanzania na dhamira ya kubadilishana uzoefu na uwezo,” alisema Mwakilishi wa India nchini Tanzania, Bishwadip Dey. “Kama wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Solar (ISA), Tanzania na India wameshirikiana katika kukuza nishati mbadala naamini ushirikiano chini ya TriDep utaimarisha ushirikiano wetu, na kusababisha ukuaji mkubwa katika sekta ya nishati mbadala ya Tanzania. Nawatakia wajumbe kutoka Tanzania safari njema yenye mafanikio na shukrani kwa Marekani kwa ushirika wao katika mpango huu.

 

Ushirikiano huu wa TriDep utawezesha gridi ya Taifa kuwa yenye nguvu na ustahimilivu zaidi nchini Tanzania. Unalenga kuboresha mifumo ya sera, kujenga uwezo wa uhakika kikanda na kuendeleza miradi mikubwa ya nishati ya jua ili kuleta nishati mbadala na ya uhakika kwa jamii za Watanzania.

 

Tuna matumaini kuwa ujuzi utakaopatikana nchini India kwa wiki mbili zijazo utaleta matokeo chanya ambayo yanaunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kuharakisha upelekaji wa nishati mbadala nchini na kusaidia ukuaji wa nishati mbadala.” alisema Naibu Katibu Mkuu wa Umeme na Nishati Mbadala, Dk. Khatibu Malimi Kazungu.

No comments:

Post a Comment

Pages