HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 05, 2025

Bajaber afungua akaunti ya mabao Simba ikiirarua Mbeya City

AKIINGIA kutokea benchi, kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba, nyota wa kimataifa wa Kenya, Mohamed Bajabr, amefunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya 'Wana Koma Kumwanya' Mbeya City FC kutoka jijini Mbeya. 


‎Timu zote zimecheza mechi hiyo kwenye dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam, zikiwa na makocha wa muda, Suleiman Matola akikaimu nafasi ya Kocha Mkuu iliyoachwa wazi na Dimitar Pantev wa Simba SC, huku Patrick Mwangata akiiongoza Mbeya City iliyomtimua Kocha Malale Khamsini.


‎Ikiwa mbele kwa uongozi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mourice Abraham (dakika ya 27) na Jonathan Sowah (38), Bajaber aliyekuwa majeruhi wa muda mrefu aliingia dakika ya 84 na ndani ya nusu dakika tu akamtungua kipa Benno Kakolanya dakika ya 85, akimalizia kimiani pasi maridadi ya Mganda Steven Mukwala.

‎Ushindi huo unaifanya Simba kuwa na asilimia 100 za ushindi, kwani imeshinda mechi ya nne mfululizo za Ligi Juu ya NBC msimu wa 2025/26, ikifikisha alama 12 na kushika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na JKT Tanzania waliojikusanyia alama 17 baada ya kucheza mechi 10.




No comments:

Post a Comment

Pages