HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2013

VURUGU ZA WANANCHI DUMILA, MKOANI MOROGORO JANA

VURUGU ZA WANANCHI KATIKA MJI MDOGO WA DUMILA, KILOSA MKOANI MOROGORO WAKIMSHIKINIKIZA MKUU WA MKOA HUO, JOEL BENDERA KUSIKILIZA KILIO CHAO CHA KUNYANYASWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA WILAYA YA KILOSA.
(PICHA ZOTE KWA HISANI JUMA MTANDA BLOGSPOT
Sehemu ya vijana wakiwa katika picha tatu tofauti mara baada ya kuchoma moto na kufunga barabara  barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kwa kuweka vizuwizi mbalimbali hali iliyopelekea watumia wa barabara hiyo kushindwa kuitumia kwa masaa matano kabla ya polisi kutuliza hali hiyo iliyoanza majira ya saa 2 asubuhi na kudumu hadi majira ya saa 7 mchana katika mji mdogo wa Dumila wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero za wakulima.
 
 Askari wa kutuliza ghasia (FFU) Morogoro wakiangalia gari mara baada ya kuharibiwa wakati wa vurugu hizo kabla ya kulinyanyua.
Hapa askari na baadhi ya raia wakiwasaidia kuinyanyua gari hili
 Gari hili likionekana mara baada ya kuharibiwa likiwa katikati ya barabara kabla ya kusukumwa na kulirejesha sehemu ambayo iliegeshwa.
 Mwananchi akizngumza jambo na askari wa kutuliza ghasia muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kuhutubia wananchi hao na amani kurejea katika hali yake ya kawaida.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO), Hamisi Selemani (kushoto) akiawaangalia vijana waliokuwa wakiimba nyimbo mbalimbali wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili awahutubie.
Rasta Man kushoto akijaribu kuwatuliza wananchi wenzake kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhutubia.
 Sehemu ya akinamama wakionyesha kukerwa na jambo wakati wa vurugu hizo, hapa walikuwa wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili kuweza kusikiliza kero zao.
 Mmoja wa vijana akitoweka na kreti la chupa tupu za soda mara baada ya kupora katika vurugu hizo.
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akiwahutubia umati wa wananchi wa vijijini vyenye migogoro ya ardhi katika tarafa ya Magole wilaya ya Kilosa kwenye uwanja wa shule ya msingi Dumila jana.
  Gari la mkoa wa Morogoro likiondoa eneo la mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la shule ya msingi Dumila wilaya ya Kilosa mkoani hapa.

VURUGU TUPU MIKOA YA MOROGORO, DAR ES SALAAM NA MTWARA.
Mmoja afariki Dumila, wengine wajeruhiwa, nyumba ya Ghasia yavunjwa Mtwara.

Kwa ufupi.
Mkoani Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60) amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa, baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu, Kilosa.

MAENEO ya mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, jana yaligeuka uwanja wa fujo na vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi.

Vurugu hizo zimehusisha wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai kwa upande mmoja wa Morogoro, Mtwara Mikindani wananchi waliizingira nyumba ya Diwani wa Kata ya Mikindani kwa madai ya kuwahifadhi watu wanaodaiwa kuwa washirikina ndani ya nyumba yake, huku Dar es Salaam eneo la Kariakoo, polisi na Wamachinga wakipambamba na Mgambo wa Jiji.

Mkoani Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60) amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa, baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu, Kilosa.

Pamoja na mauaji hayo, wasafiri waliokuwa wakitumia Barabara ya Morogoro – Dodoma, nao walionja machungu ya vurugu hizo, baada ya kukwama kwa saa 5 kutokana na wananchi wa kijiji hicho, kufunga barabara kwa mawe, magogo ya miti na kuchoma magurudumu ya gari.

Wananchi hao walichukua hatua hiyo huku wakisisitiza kutaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ili kumaliza mvutano huo.

Katika vurugu hizo wanakijiji hao walivunja vioo vya madirisha ya baadhi ya nyumba tano za kulala wageni, kuharibu gari dogo aina ya Landcruser pamoja na kupora mali mbalimbali zi nazodaiwa kumilikiwa na wafanyabiashara wa jamii ya Kimasai.

Kabla ya kufanya uharibifu huo saa 2:30 asubuhi, wananchi hao walifanya maandamano sambamba na kusimama katikati ya barabara, hali iliyosababisha polisi kufika eneo hilo kwa ajili ya kuwadhibiti.

Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), walifika eneo la tukio 5:20 asubuhi na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi, hatimaye kufungua barabara hiyo.

Pamoja na barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, wananchi hao pia walifunga barabara ya Dumila- Kilosa, hivyo kuyafanya magari yaliyokuwa yakitumia barabara hiyo kukwama kwa zaidi ya saa sita na kusababisha usumbufu kwa wasafiri waliokuwa wakitumia barabara hiyo.

Wakati vurugu hizo zikiendelea, wafugaji wa jamii ya Kimasai wakiwamo wanawake na watoto walionekana kukimbilia kwenye kituo kidogo cha Polisi Dumila kwa lengo la kujihami na kupata msaada wa polisi kutokana na hofu ya kushambuliwa na wananchi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo kwenye eneo la tukio, mkulima aliyefahamika kwa jina Mauya Hamadi alisema kuwa wananchi wamelazimika kufanya vurugu hizo baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai kuingiza mifugo kwenye mashamba ambayo tayari yameshapandwa mazao na kufanya uharibifu.

Alisema kuwa tayari suala hilo walishalifikisha kwa uongozi wa kijiji, kata, wilaya hadi mkoa, lakini hakuna jitihada zozote zinazofanywa na viongozi, hivyo kulazimika kumtaka Mkuu wa Mkoa Joel Bendera, kwenda kuzungumzia suala hilo, ambapo hata hivyo mkuu huyo wa mkoa hakuwahi kufika eneo hilo hadi walipoamua kufanya maandamano hayo.

1 comment:

  1. bila nguvu kutumika haki haiwezi kupatikana

    ReplyDelete

Pages