HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2013

AFCON 2013: IVORY COAST, TUNISIA VITANI LEO

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

Ivory Coast na Tunisia zote zinaongoza kundi kwa tofauti ya mabao, baada ya zote kushinda mechi zao za ufunguzi, ambapo Tembo waliichapa Togo mabao 2-1, huku Tunisia wakiwalaza Algeria kwa bao 1-0

TEMBO wa Ivory Coast leo wanashuka kwenye dimba la Royal Bafokeng kuumana na Tunisia, huku mshindi wa pambano hilo akitarajiwa kujikatia tiketi ya robo fainali kutokea kundi D – mechi moja kabla ya kumaliza hatua ya makundi.

Tiketi ya robo fainali kwa mshindi wa mechi hii itategemea na matokeo ya sare katika mechi nyingine jijini Rustenburg, baina ya Algeria na Togo itakayochezwa baada ya Ivory Coast na Tunisia kumaliza vita yao.

Ivory Coast na Tunisia zote zinaongoza kundi kwa tofauti ya mabao, baada ya zote kushinda mechi zao za ufunguzi, ambapo Tembo waliichapa Togo mabao 2-1, huku Tunisia wakiwalaza Algeria kwa bao 1-0.

Ivory Coast ina kibarua kigumu cha kusawazisha kiwango chao dimbani kuweza kurejesha amani mioyoni mwa mashabiki wao, baada ya kuliwa kooni katika pambano lao la Jumatatu lilioonekana kama kutaka kumalizika kwa sare.

Mwanamichezo Bora wa Mwaka wa Afrika wa BBC, Yaya Toure, aklifunga bao la mapema, kabla ya Jonathan Ayite kuisawazishia Togo, kabla ya Gervinho kuipa ushindi dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho na kuambulia pointi tatu muhimu.

No comments:

Post a Comment

Pages