HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2013

Askari Polisi Mtwara watimuliwa uraiani


Askari wa jeshi la polisi mkoani Mtwara wapo katika hali mbaya ya kuishi baada ya kutimuliwa toka uraiani  na kulazimishwa kuishi kambini, baada ya kutofautiana na wananchi katika sakata la gesi lililofanya Askari kuelekezwa kukamata na kupiga baadhi ya wananchi.

Chanzo chetu cha habari kimethibitisha kuwa tarehe 17 June wiki iliyopita kamati ya Ulinzi  na Usalama ya mkoa ilifanya kikao ikiwa na baadhi ya viongozi wa jeshi la wananchi, na viongozi mbalimbali wa serikali, walimwomba Kamanda wa polisi wa mkoa Linus Sinzumwa kuomba radhi kwa niaba ya Askari wake waliofanya vitendo vya kihalifu dhidi ya raia.

Katika sakata hilo wananchi hawakukubali, badala yake waliwaomba Askari wote wahame uraiani wakaishi kwenye kambi zao na nyumba zao ambazo kimsingi hazitoshi kuwezesha malazi kwa Askari wote.

Taarifa zaidi zinasema Askari walioko Mtwara wamelazimika kuishi katika mahema waliyogawiwa na kuyaweka katika maeneo ya Line polisi, mahali ambapo wanadhani ndio salama kwao.


Uhusiano kati ya jeshi la polisi na raia unadaiwa kutetereka hadi kutouziwa baadhi ya bidhaa muhimu kwa ajili ya chakula, na raia yeyote anayebainika kutumwa kununua kwa ajili ya askari anaadhibiwa na raia wenzake.

No comments:

Post a Comment

Pages