HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2014

'I DO' YA DYNA KUTUA SOKONI KESHO

Na Elizabeth John

MWANADADA ambaye anatamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Dyna Nyange ‘Dyna’ leo anatarajia kusambaza video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘I Do’.



Video ya wimbo huo ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, imetengenezwa na mtayarishaji wa hapa nyumbani ambaye Dyna hakutaka kumuweka wazi na kuwataka watazamaji kukaa mkao wa kula kuitazama.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Dyna alisema video ya kazi hiyo ameifanyia nyumbani kwasababu ameona kuna uwezekano huo hivyo amewataka wasanii wenzie kutofuata mkumbo kwenda kufanyia video nje ya nchi.

“Tanzania kuna uwezekano wa kufanya video nzuri, kama umeona Dar es Salaam hamna mazingira unaweza kwenda hata mikoani sio lazima uende nje ya nchi tunatakiwa kuvithamini vya kwetu kwanza,” alisema.

Dyna amewataka wapenzi wa kazi zake kukaa mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo anasema itakuwa ni moto wa kuotea mbali kutokana na mazingira ambayo ametumia kupiga picha kazi hiyo.


Aliongeza kuwa, mfalme wa video hiyo ni Nando ambaye amewahi kushiriki mashindano ya Big Brother Afrika (BBA).

No comments:

Post a Comment

Pages