HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 30, 2015

UMOJA WA VIJANA WA CUF WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZURU

Mwenyekiti wa Vijana CUF Taifa Hamidu Bobali akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kitendo cha kudhalilishwa kwa Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba Januari 27 wakati walipokua wanaandamana kwa ajili ya kuwakumbuka wanachama wenzao ambao waliuawa na kuteswa mwaka 2001 huko Zanzibar. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana CUF, Wilaya ya Kinondoni, Aboubakari Kabambura na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana CUF Taifa, Maulid Said. (Picha na Francis Dande)


Na Mwandishi Wetu

JUMUIYA ya Vijana ya Chama cha Wananchi (JUVICUF) wamelaani vikali kitendo walichokiita cha kinyama kilichofanywa na Jeshi la Polisi  kumdhalilisha Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba na Viongozi waandamizi wa Chama wa Ngazi ya Taifa na wilaya.


Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Vijana CUF, Taifa Hamidu Bobali alisema kuwa kitendo cha kudhalilishwa kwa Mwenyekiti wao pamoja na wanachama wengine ni unyonyaji wa demokrasia.

Mwenyekiti wa CUF na wanachama wengine walifanyiwa unyanyasaji na udhalilishaji huo Januari 27 wakati walipokua wanaandamana kwa ajili ya kuwakumbuka wanachama wenzao ambao waliuawa na kuteswa mwaka 2001 huko Zanzibar.

Kutokana na hali hiyo Vijana CUF wamemtaka waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mathius Chikawe kujiuzuru kutokana na tukio hilo sambamba na kauli waliyoiita kuwa ya uongo aliyoitoa bungeni.
Jumuiya hiyo imeazimia kuandaa maandamano makubwa ya kulaani vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu zinazofanywa na Serikali ya CCM kupitia Jeshi lake.


Bobali alisema kuwa wanamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu kuona aibu na na kutokubali kuacha wananchi waendelee kuliona jeshi hilo kuwa limekosa watu wanaoweza kujenga hoja mbele ya umma.

Katika hatua nyingine wameitaka Serikali izifute kesi zote zilizotokana na tukio hilo la Januari 27 mwaka huu.

"IGP akanushe taarifa ambayo JUVICUF tunaiona ni kauli ya kitoto na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa kama kama Chagonja ameudhihirishia Umma kuwa Jeshi la Polisi lilikosa sababu ya kuzia maandamano ya CUF badala yake bila kuona aibu anaibuka na hoja za kitoto zilizokosa mashiko,alisema Bobali".

Alisema hoja ya kuibiwa silaha kwenye kituo cha Polisi Ikwiriri hakina mahusiano yeyote na kufanyika kwa maandamano CUF na isitoshe CCM wameandaa maandamano Songea katika kuazimisha tarehe ya kuanzishwa kwa CCM wakiwa wamesafiri wajumbe wa chama hicho hadi Songea.

Vijana hao walitoa onyo kwa viongozu wa CCM juu ya kuamrishwa kuzalilishwa kwa viongozi wa CUF na kwamba hawatokaa kimya katika kujibu mapigo juu ya viongozi wa CCM.

No comments:

Post a Comment

Pages