HABARI MSETO (HEADER)

Breaking

November 13, 2015

Wakazi wa jijini Dar es Salaam wafurika Ufukwe wa Coco Beach kujionea Samaki mkubwa aina ya Nyangumi

Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya samaki mkubwa jamii ya nyangumi anayekadiriwa kuwa na tani 20 aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam. Wakazi hao waliofika katika eneo hilo huku wakiwa na vyombo vya kubebea mafuta ya samaki huyo. Mashuhuda hao walisema kuwa mafuta yake ni dawa ya watoto, hata hivyo wataalam wa afya hawakuweza kupatikana kuelezea usalama wa nyama ya samaki huo pamoja na mafuta yake.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay Zefrin Lubuva alizitaka mamlaka zinazohusika na afya kufika na kuthibitisha usalama wa kitoweo hicho kwa afya za wakazi hao.  (Picha na Francis Dande)

 Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya Samaki mkubwa jamii ya Nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa jijini Dar es Salaam wakijipatia kitoweo na mafuta ya Samaki mkubwa jamii ya Nyangumi aliyeonekana Novemba 13 katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages