HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2016

SNURA AOMBA RADHI WATANZANIA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Snura Antony Mushi amewaomba radhi watanzania kwa nyimbo yake ya Chura ambayo imepigwa marufuku na Serikali kutokana na wimbo huo kumdhalilisha mwanamke.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo huku akiambatana na Meneja wake, Hemed Kavu 'HK' Snura amesema kuwa anaomba radhi kwa serikali ambayo ndio inayosimamia sekta ya sanaa kwa kutofuatilia sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa muziki wa sanaa hapa nchini.

Aidha Snura aliongeza kuwa "Mimi na Meneja wangu tunaahidi kutorudia tena kufanya kosa kama hilo la udhalilishaji na iwapo tutarudia bas i tupewe adhabu kali na mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa sheria" na kuahidi kuwa mfano bora kwa jamii inayowazunguka na kwa wasanii wenzake katika masuala yanayohusu kutunza na kufuata maadili na utamaduni wa mtanzania.

Kutokana na sakata hilo ambapo Serikali ilisitisha shughuli za msanii huyo mpaka taratibu za kujisajili katika Baraza la Sanaa  la Taifa (BASATA) zitakapokamilika, Snura alisema kuwa tayari ameshajisajili katika Baraza jilo na kupata cheti kinachomruhusu kufanya shughuli za muziki wakati wowote kuanzia leo baada ya kupata usajili huo
 Snura Mushi akionyesha cheti alichokabidhiwa na Basata baada ya kujisajili katika baraza hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande)
Meneja wa msanii wa kizazi kipya Snura Mushi, Hemed Kavu.
 Waandishi wa habari wakiwa kazini.
 Msanii wa muziki wa kipya, Sunra Mushi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Pages