Wachezaji
wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Ivory Coast, wakiwa katika
mazoezi ya kujianda na mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la
Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 26 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam. (Picha na Francis Dande)
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Ivory Coast, imeingia
Dar es Salaam, Tanzania leo saa 8.00 usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege
la Ethiopia ikitokea jijini Abidjan.
Timu hiyo imekuja Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa
kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu
wa ufukweni ambako itacheza na wenyeji Tanzania Ijumaa wiki hii kwenye
uwanja maalumu ulioandaliwa kwa ajili ya mchezo huo.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic
Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na
Muhammad Ssenteza.
Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku
Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. Timu hizo zinatarajiwa
kucheza mechi mbili za kuwania kufuzu kwani mara baada ya mchezo wa Dar
es Salaam, zitarudiana tena Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa
amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kwa upande wa Tanzania, Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Mwansasu,
anaendelea na mazoezi na wachezaji wake 16 aliowatangaza wiki iliyopita.
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania
Bara.
Wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahmad, Mohammed Makame,
Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka
Zanzibar.
Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland
Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma
Juma na Kevin Baraka.
No comments:
Post a Comment