HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 29, 2016

ZEC: WATU 6743 HAWANA SIFA ZA KUPIGA KURA ZANIZIBAR

Na Talib Ussi, Zanzibar

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakusudia kuwafuta wapiga kura  6743 katika daftar la wapiga kura kwa madai kuwa wamepoteza sifa za kuwemo humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Tume hiyo Salum Kasim Ali alisema kuwa kupitia katika afisi zao zilioko mawilayani imegundua watu hao kutokana na sababu tofauti.

Alisema watu 2765 ni wanawake na 3978 ni wanaume ambao alidai walibandikwa katika shehia tofauti visiwani hapa ili watu waweze kujirisha nao.

Alifahamisha kuwa wapiga kura hao walipoteza sifa ama kwa kufariki au kuhama sehemu moja kwenda nyengine.
Alichanganua kwa mujibu wa wilaya zote za Zanzibar ambapo Wilaya ya mjini ungujajumla ya wapiga kura 1928, Wilaya za Magharibi A na B 785  ambapo Kaskazini A 1450 na Kaskazini B 210.

Wilaya kati Unguja 290 na Kusini Unguja ni 415, pamoja nan  micheweni katika Kisiwa cha Pemba 135, wakati Wete 332, Chake Chake 562 na Wilaya ya Mkoani Pemba 636.

Salum alieeleza waandishi wa habari kuwa lengo la kufanya kazi hiyo ni kuboresha Daftari hilo ili liende na wakati bila ya kuwepo na kasoro zisizo za lazima.

No comments:

Post a Comment

Pages