HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 11, 2017

MAMLAKA YA ELIMU YAIPIGA TAFU UDSM SH. MIL. 496


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), (katikati), Graceana Shirima akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makubaliano ya ujenzi wa uzio wa Hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere amabapo TEA ilitoa Sh. Mil 496 kwa ajili ya ujenzi wa uzio huo. Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara. (Picha na Francis Dande).

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara katika hafla hiyo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), (katikati), Graceana Shirima akisaini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa uzio wa Hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara wenye thamani ya Shs. Milioni 496. Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Meneja Ufadhili wa Miradi, Anne Mulimuka. 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), (katikati), Graceana Shirima akibadilishana hati ya makubaliano ya ujenzi wa uzio wa Hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara.

 Kaimu Meneja Ufadhili wa Miradi TEA, Anne Mulimuka akisaini.

 Kaimu Mwanasheri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Saudin Mwakaje akisaini.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima wakionesha mkataba waliosaini.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara na  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima wakionesha mkataba waliosaini leo.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima akibadilishana hati na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara wakionesha furaha yao baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere.

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandara akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa uzio wa hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Picha ya pamoja.

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa utekelezaji kwa ajili ya kujenga uzio kuzunguka hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaan na Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mkukandara.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Shirima alisema jumla ya sh. 496,646,868 zitatumika kujenga uzio huo kuzunguka hosteli mpya zinazojengwa pembezoni mwa barabara ya Sam Nujoma.

"Tunatarajia utekelezaji wa mradi huu utakamilika katika kipindi cha miezi 12 kutoka sasa. Tunalenga kuwafanya wanafunzi hasa wasichana watakaoishi kwenye hosteli hizo kuwa salama," alisema Shirima.

Alisema mamlaka yake inatekeleza miradi mbalimbali kwa kushirikiana na UDSM ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya mihadhara, ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada, vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na ufadhili wa mafunzo ya awali kabla ya kujiunga na chuo hicho.

Akishukuru baada ya kusaini mkataba huo, Profesa Mukandara alisema ujenzi huo utachochea kasi ya kusoma kwa wanafunzi kwa kuwa eneo hilo litakuwa tulivu.

Pale zinapojengwa hosteli ni eneo lililozungukwa na maeneo yenye mikusanyiko ya watu wakiwemo wanaokwenda kufanya mazoezi na kuogelea kwenye viwanja vya chuo hicho.

"Kukamilika kwa hosteli hizo zinazotarajiwa kuchukua wanafunzi 6,000 kwa wakati mmoja zaidi ya nusu ya watakaoishi hapo watakuwa wanafunzi wa kike," alisema Makamu Mkuu huyo wa UDSM.

No comments:

Post a Comment

Pages