HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 11, 2017

KONGAMANO LA PILI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI LAFANYIKA MKOANI DODOMA

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika leo mjini Dodoma . TSNwalikuwa mmoja wa wadhamini. Dk Yonazi alisema kuwa ili kuwaezesha wananchi kiuchumi ni lazima jamii ihabarishwe juu ya fursa mbalimbali zilizopo, lakini pia muhimu wa sekta binafsi kuwa na ubunifu na mifumo ya kujitengenezea utajiri. Picha zote na Mroki Mroki-dailynewstzonline.blog
Afisa Mtendaji Mkuu wa MM Maxcom , Juma Rajab akielezea uzoefu wake na kusema kuwa inahitajika kuwawezesha wajasiriamali wote, wadogo, wa kati na wakubwa ili kufanikisha wananchi kuweza kuingia katika uchumi wa viwanda. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mada juu ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema ni vyema viongozi na jamii ikawana na utaratibu wa kuchapa kazi ili iweze kufanikiwa katika suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Wakuu wa Mikoa, Amos Makala (kulia) na John Mongela wakifuatilia kongamano hilo. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.

No comments:

Post a Comment

Pages