Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

TAA YAFANYA MKUTANO WA WAFANYAKAZI

Mohamed Mpuku mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), akiuliza swali kwenye mkutano wa wafanyakazi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Transit TB I, ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mahala pa kazi iliyoanza Juni 16-23.
Musso John wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), aliyesimama akiwasilisha hoja zake leo kwa meza kuu wakati Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mtengela Hanga alipokutana na wafanyakazi kwenye ukumbi wa Transit TB I, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
Mastidia Ndomulwango akiwasilisha mapendekezo yake kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mtengela Hanga, katika mkutano wa wafanyakazi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Transit TBI, katika Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mtengela Hanga (kushoto), akijibu hoja za wafanyakazi wa mamlaka hiyo leo alipokutana nao katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Transit TB I, katika muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma itakayomalizika Juni 23.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Ally Mohamed (mwenye kipaza sauti), akifafanua mojawapo ya maswali yaliyoulizwa na wafanyakazi wa mamlaka hiyo, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Transit TBI, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Joseph Nyahende (aliyesimama), akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yaliyoulizwa na wafanyakazi walioudhuria mkutano ulioitishwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mtengela Hanga, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, itakayomalizika Juni 23.

No comments:

Post a Comment