HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 11, 2017

TAMWA Wakabidhi vyerahani kwa wajasiriamali

Na Talib Ussi, Zanzibar

Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA) upande wa Zanzibar kimetoa msaada wa vyerahani sita kwa ajili ya kushonea vitu vigumu kwa wajasiriamali mbali mbali visiwani humu.

Makabidhiano hayo yalifanyika Juzi huko katika afisi ya Chama hicho Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja ambapo wajasiriamali baadhi ya waliopokea kwa niaba ya wenzao.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa TAMWA- Zanzibar Dr. Mzuri Issa Ali aliwataka wajasiriamalli hao kuzitunza mashine hizo ili zilete mafanikio yaliokusudiwa.

Alisema lengo la kutoa misaada hiyo ni kutaka kuona wajasiriamali hasa akina mama wanaendelea na kuepukana na utegemezi katika kuendesha maisha yao.

“Sio utegemezi tuu lakini hata pale wanapopata oda ya mikoba au Vipochi waweza kutimiza oda kwa wakati uliopangwa” alisema Dk. Mzuri.

Vyerahani hizo sita ambazo ni maalumu kwa kushonea vitu Vigumu vinathamani ya milioni tano na laki moja.

Wakitoa shukrani zao baada ya kupokea msaada huo, kwa niaba ya vikundi vyengine Nassira Salum Ahmed kutoka kikundi cha Kiuyu Minungwini Mkoa wa Kaskazini Pemba alieleza kuwa kupokea vifaa hivyo ni sawa na kuondoa chamoto zilizozikiwakabili kwa asilimia nyingi.

“Nna imani hata nipate oda ya mikoba 1000 moja sasa naweza kuitimiza tena kwa muda mfupi tu” alieleza Bi Nassira.

Kutolewa kwa vyerahani hivyo ni muendelezo wa mradi wa kuwawezesha wanawake kiuchumi (WEZA II) ambao uliza mwaka 2008 hada 2011 kwa weza I na weza II unaendelea ambapo Wanawake zaidi ya 7000 kupitia vikundi zaidi ya mia tatu wamefaidika na mradi huo.

Mradi huo wa weza II unaendeshwa kwa mashirikiano baina ya Tamwa, Zanzibar na Zanzibar Milele Foundationpamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Msitu wa Jonzani(JOCDO) na shirika la Kuweka na Kukopa (PESACA)

No comments:

Post a Comment

Pages