HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 12, 2018

Mwenyekiti Mtendaji mpya Fastjet aanika mikakati ya umiliki

 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo kuhusu uteuzi mpya wa Mwenyekiti Mpya wa Fastjet Tanzania Lawrence Masha. Pichani wengine ni Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Fastjet Tanzania, Lawrence Masha na Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.
Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Shirika la Ndege  Fastjet Tanzania, Lawrence Masha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo kuhusu uteuzi wake wa kuwa mwenyekiti wa shirika hilo. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI Mtendaji mpya wa Shirika la Ndege la Fastjet Airlines Ltd, Tanzania, ameelezea mikakati madhubuti ya kuendelea kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi, ikiwa kama kampuni inayomilikiwa na Watanzania pamoja na masoko ya talii za nje.

Novemba 6 mwaka huu, Fastjet ilimteua Lawrence Masha kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kwanza wa shirika hilo, uteuzi ambao umethibitisha nia ya kimkakati ya Fastjet kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi kulingana na uwezo na pato la Mtanzania.

Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Masha alisema: “Tumejikita zaidi kwa Watanzania ambao wamefaidika kutokana na huduma zetu kwa miaka sita sasa. Tunatarajia kuongeza safari za ndani na pia kuongeza idadi ya ndege ambazo zinakidhi mahitaji ya soko.

“Tunaona fursa kufanya kazi na kushirikiana na mashirika ya ndege za ndani na nje ya nchi pamoja na Air Tanzania kutimiza mikakati ya Serikati ya utalii,” alisema Masha.
Imeelezwa kuwa, kati ya mashirika ya ndege yanazokua kwa kasi zaidi, Fastjet Airlines Ltd, Tanzania, ambayo imetoa huduma kwa miaka sita, ikiwa imesafirisha zaidi ya abiria milioni 2.5 ndani ya Tanzania pekee.

Fastjet, lenye bei nafuu, linahudumia usafiri wa ndege katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lusaka na Zimbabwe, ambako lina rekodi ya kusafirisha wastani wa abiria 30,000 kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment

Pages