HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2021

UWEKEZAJI WENYE KUZINGATIA UTAALAMU

 

UWEKEZAJI MSETO UNAOZINGATIA UTAALAMU WA HALI YA JUU

Uwekezaji wa pamoja ni aina ya uwekezaji unao vuta watu na makampuni mbalimbali kuchanga pesa zao katika mfuko mmoja kwa viwango tofauti tofauti, na kumkabidhi meneja awekeze kwa niaba yao. Pesa huwekezwa katika mfumo wa vipande; na meneja huwekeza kwa kufuata masharti na kanuni husika. Meneja anakuwa mtu au kampuni iliyo bobea kwenye fani ya uwekezaji wa pamoja.

Kawaida mfuko huwa na malengo mbali mbali, hivyo meneja anawekeza huku akihakikisha analenga malengo husika ya mfuko kwani malengo ndiyo yanavuta wawekezaji. Mfano lengo linaweza kuwa elimu kwa watoto, kukuza mtaji, kupata gawio au kupata faida ya bima pamoja na uwekezaji. Kazi kuu ya meneja ni kutunisha mitaji na vipato vya wawekezaji wake huku akifuata kanuni na misingi kama ilivyo elekezwa kwenye waraka wa makubaliano.

Uwekezaji wa pamoja unawapa nafasi wawekezaji wenye kipato kidogo na kikubwa uwezo wa kushiri kwenye masoko ya fedha na mitaji. Sio rahisi mtu mwenye hela kidogo kama shilingi 10,000, 20,000, 50,000 kushiriki kwanye masoko ya hisa, au kwenye hati fungani lakini kupitia uwekezaji wa pamoja inawezekani bila tabu, hivyo mifuko ya uwekezaji wa pamoja inatoa uwezeko kwa wasio na uwezo kushiriki kwenye soko la hisa na hata hati fungani kwa maneno mengine wananchi wanapata fursa sawa kushiriki kwenye masoko ya fedha na masoko ya mitaji. Kwa hiyo fedha zinakusanywa kutoka katika hadhara halafu zinawekezwa kwenye soko la hisa, soko la hisa lina kampuni mbali mbali hii ina maana kuwa meneja ananunua hisa anazoona zinafaa; meneja pia ananunua dhamana za serekali (hati fungani) ambapo ni mkopo kwa serekali wa muda mfupi au mrefu. Kwa kufanya hivyo atapata faida kama hisa zimepanda bei wakati mwingine anaweza pata hasara kama hisa hazijafanya vizuri lakini anatumia utaalamu ili kupunguza uwezekano wa kuanguka, na hapo hapo atapata faida kutokana na mkopo kwa serekali kupitia hati fungani. Hizi hela sio za meneja ni za wawekazi menaja analipwa asimilia kama ilivyo ainishwa kwenye makubaliano yaliyoyomo kwenye waraka husika.

Ukiwekeza kwenye hisa moja kwa moja ni tofauti na kama umewekeza kupitia kwenye kampuni ya uwekezaji kama vile UTT AMIS.  Uki nunua hisa unakuwa umenunua kampuni husika ukinunua vipaande unakuwa ni sehemu ya uwekezaji wa kampuni husika lakini huimiliki hiyo kampuni. Mwenye hisa ana turufu mkononi lakini mwenye kipande hana. Lakini hisa huwa ni za kampuni moja. Kipande cha kwenye kampuni ya uwekezaji wa pamoja kinawakilisha mchanganyiko wa sehemu mbali mbali mfano hisa za kampuni nyingi, akaunti za muda maalumu, mikopo kwa serekali ya muda mfupi na muda mrefu n.k. ; kwa mantiki hii kipande ni uwekezaji ulio tawanywa sehemu nyingi na hii ni faida kwa mwekezaji, kwani sehemu moja ikianguka sehemu nyingine inafidia.

Chukulia mwekezaji anayewekaza kwa kununua hisa za kampuni ABC za shilingi 1,000,000 huyu atapata hasara kama kampuni hii itaanguka. Lakini kama akiwekeza kupitia uwekeza wa pamoja ina maana kwa kiwango chake hicho hicho cha pesa yaani shilingi 1,000,000 itagawanywa kwa mfano kwa kampuni ABC shs 100,000, kampuni XYZ shilingi 200,000, Hati fungani shs 300,000 akaunti za muda maalumu shilingi 200,000 na kampuni  NZY shilingi 200,000   hii ina maana ya kuwa kwa hisa peke yake (ABC)  milioni moja, lakini kwa uwekezaji wa pamoja ile milioni  moja kaitawanya.

Ikatokea kwamba kampuni ABC imeanguka ina maana kuwa mwekezaji atakuwa amepoteza kila kitu kwenye hii kampuni kama angekuwa mayayi yote (mtaji) wote kauweka hapo.

Lakini kwenye uwekezaji wa pamoja atakuwa amepoteza shilingi 100,000 tu ambazo zitafidiwa na hizo sehemu zingine ambazo hazikupata misuko suko.

Mambo ya muhimu kukumbuka

1.   Uwekezaji wa pamoja ni uwekezaji mseto unaozingatia utaalamu wa hali ya juu.

2.   Uwekezaji wa pamoja uko katika msingi wa kutawanya athari za uwekezaji- mayayi hayakai kwenye  kapu moja.

3.   Uwekezaji wapamoja uko katika misingi ya utaalamu mkubwa, uwazi na ni rahisi mtu yeyote kushiriki.

4.   Mifuko ya uwekezaji wa pamoja inaweza kuwa ya hati fungani peke yake au mchanganyiko wa hisa na hati fungani na bidhaa zingine za masoko ya fedha. Pia yaweza kuwa ya uwekezaji kwenye hisa peke yake.

5.   Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ina nafuu ya kodi na ina gharama nafuu kiuendeshaji.

6.   Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni chombo muhimu cha kukuwezesha uwe na maisha mazuri kabla na baada ya kustaafu.

Faida kwa mwekezaji

Gawio –Meneja wa mfuko analipa faida inayo patikana kutoka kwenye uwekezaji  kwa wawekezaji kama ilivyo ainishwa kwenye waraka wa makubaliano.

Kukuza mtaji-Wakati mwingine mwekezaji anaweza kuchaguwa kuto kuchukuwa faida na kuiacha izidi kukuwa zaidi. Yaani mpango wa kukuza mtaji.

Kama meneja kawekeza katika mfuko wa hisa na thamani ya hisa ikapanda na mwekezaji akataka pesa zake, meneja atanunua hizo hisa au ataziuza hivyo basi mwekezaji akafaidika na ongezeko.

Pia mwekezaji anaweza kuchagua kuchukuwa faida tu, huku akiacha uwekezaji wake ukiendelea kutengeneza pesa.

 Mifuko ya uwekezaji iko ya aina nyingi kulingana na malengo ina malengo tofauti. Kuna mifuko ina faida sana lakini mambo yakiwa mabaya hasara huwa kubwa pia, kuna mifuko ina faida nzuri na ya wastani lakini athari kama hazipo au ni ndogo  sana.

Kuna uwekezaji katika maeneo mbali mbali, ila kwa hapa nchini kuna sehemu kubwa tatu ambapo mifuko huwekeza.

Kama ilivyo ainanishwa hapo mwanzo kuna mifuko inawekeza kwenye hisa tu. Hisa nazo zime gawanyika mfano za kampuni za ndani ya nchi au nje ya nchi au mchanganyiko. Za kampuni ndogo au kubwa, kampuni zinazo anza au za zamani n.k

Kuna mifuko inawekeza kwenye  kukopehsa kwa muda maalumu kwa mfano ukinunua hati fungani za serekali, au ukiwekeza katika akaunti za muda maalumu kwenye benki utapata faida ambayo inakuwa ni ongezeko kwenye uwekezaji wako.

Tukumbuke kuwa hati fungani ziko za aina tofauti za serekali na hata kampuni binafsi.

Na pia kuna mifuko ambayo hufanya uwekezaji mseto. Yaani uwekezaji kwenye masoko ya mitaji (hisa na hati fungani za muda mrefu) na pia kwenye masoko ya fedha –kwenye mabenki, akaunti za muda maalumu na hati fungani za muda usio zidi mwaka mmoja.

Pamoja na faida za uwekezaji wa pamoja ambazo zimetajwa humu ambazo ni pamoja na urahisi wa kupata pesa zako, ukihitaji pesa zako tu unalipwa ndani ya muda mfupi sana- ukwasi umezingatiwa kwa kiwango cha juu, kutawanya athari za uwekezaji na utaalamu katika kusimamia na kuwekeza hii ina maana mifuko ya uwekezaji wa pamoja inafaa vijana, watu wa umri wa kati na hata wazee. Uwekezaji wa pamoja pia unarahisisha ukwasi unanunua  vipande na kuviuza wakati wowote sio kama akaunti za muda maalumu ukisha wekeza huna budi kusubiri mpaka muda wa makubaliaona ufike, chini ya hapo umevunja masharti. Kama una hisa ndani kuziuza inaweza kuwa ngumu hususan kama hisa ulizo nazo ni za kampuni ambayo haitengenezi faida lakini kipande unanunua na kuuza muda wowote.

 Hasara au changamoto nazo zipo ikiwa kama, thamani ya kipande hupanda na kushuka , thamani ikipanda inakuwa ni habari nzuri, ikishuka inakuwa ni habari mbaya. Lakini kwa mwekezaji madhubuti tambua bila kuthubutu si rahisi kupata. Wanasema waswahili hakuna pesa za bure. Kumbuka uwekezaji wowote lazima kuwe na kupanda na kushuka, milima na mabonde.

Uwekezaji wa pamoja unavuta hela nyingi kutoka kwa watu wengi kila siku; kila siku kuna watu wanaweka fedha na kila siku kuna watu wanatoa pesa kwa ajili ya matumizi yao mbali mbali. Ili kuwa na uhakika kuwa kila siku unaweza kulipa fedha za wawekezaji kutokana na matakwa yao ni lazima meneja atenge kiasi fulani kufanikisha hitaji hili la kutoa pesa bila kumbughudhi mwekezaji. Kuwa na pesa nyingi amabazo zinasubiri kulipa ni jambo zuri lakini ki uwekezaji ni changamoto kwani pesa hizi zingekuwa ndani ya uwekezaji zingeleta faida zaidi ya kuwa zimekaa tu zikisubiri kulipwa kwa wawekezaji wenye kuzihitaji.

Gharama za meneja na matumizi mengi sio kubwa sana lakini gharama hizi zaweza kuwa mzigo kwa mfuko kama thamani ya vipande inashuka. Kwa bahati nzuri uwekezaji kupitia UTT AMIS umekuwa wa makini na wenye faida; hili limekuwa si tatizo hususan katika muda wa kati na muda mrefu.

Jambo linguine meneja anatakiwa ni kutokuwa na mifuko mingi inayo fanana, na pia kuhakikisha kuwa hatawanyi sana katika kuwekeza, yaani tawanya kiasi kwani hata sukari ukiitia maji mengi utamu hupotea. Dhumuni la mfuko lazima liwe linaeleweka vizuri na kiwango cha utawanyaji katika sehemu za kuwekeza lazima kitafutwe kisomi ili kuleta kiwango cha juu cha faida tarajiwa. Ni changamoto  kwamtu binafi kuwa na ujuzi wa kutawanya uwekeaji.

Kwa mantiki hii basi ya kutawanya athari za uwekezaji wa pamoja sehemu mbali mbali, na kwa kutumia uzoefu na utaalamu, hofu ya mwekezaji kupoteza inakuwa imezingatiwa. Wawekezaji wengi wanajiuliza kipi bora, mfano kwenye kuchagua hisa wawekeze wenyewe moja kwa moja au wapitie kwa meneja au dalali, ni ukweli kuwa hata wakati wa misuko suko meneja lazima alipwe, lakini ni ukweli zaidi kuwa meneja ana uzoefu na ujuzi na kwa yeye hii ndiyo kazi yake. Pengine mwekezaji ni mfanya biashara au mkulima hii ina maana kuwa hati fungani au hisa si sehemu ya maisha yake lakini kwa kampuni kama UTT AMIS haya ndiyo maisha yake.

Kuhusu kupanda au kushuka kwa thamani ya vipande  kutokana na hali ya soko; swali la kujiuliza ni Uwekezaji upi ambao kila siku unapanda tu bila kushuka?

Tukumbuke kuwa tukiwekeza UTT AMIS Uwekezaji wetu unasimamiwa na mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA), huku kukiwa na mwangalizi ambaye ni benki ya CRDB, na pia huku wakiwepo wakaguzi wa maheseba, wana sheria, na kampuni yenyewe ikiwa ni ya Serekali chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Pia Uwekezaji wa pamoja unasimamiwa kitaalamu. Kwa mawazo ya mwandishi wa Makala hii hapa ni sehemu ambapo kila mwenye nia ya kuwekeza angethubutu kwani tahadhari za hali ya juu huchukuliwa.

Bado watu wengi wanahifadhi hela katika mifumo ya zamani, kama vile kwenye kibubu, au hata kuzichimbia sehemu Fulani hivi, ambapo haziwapi faida yeyote na bado usalama wake unakuwa mdogo zaidi ya ile tahadhari ya kipande kupanda au kushuka. Na hata pale tunapoweka sehemu rasmi kama vile taasisi za kifedha ni vizuri kujiuliza je tutapata faida linganishi? Mpaka mwaka 2014 kiwango cha watu waliokuwa wanaweka fedha kwenye mfumo rasmi walikuwa wastani wa aslimia 16 katika nchi za afrika mashariki na kati na Tanzania ilikuwa bado haijafika asilimia 10, hii ina maana kuwa bado elimu inahitajika kwanza ya kuweka halafu ya kuwekeza ili walau kupandisha kiwango hiki juu kwa faida ya watu nan chi zao.

Shukrani kwa kampuni za simu kwani wameongeza kiwango hiki na kwenda juu kwani watu wengi wanashiriki katika mfumo wa kuweka, kulipa, na hata huduma nyingine nyingi za kifedha kupitia simu za kiganjani.

Moja wapo ya majukumu makubwa UTT AMIS ni kuanzisha na kuhamasisha ikiwa ni pamoja na kusimamia Uwekezaji wa pamoja, na ni nia ya UTT AMIS kuhakikisha kuwa dhana nzima ya Uwekezaji wa pamoja inaelewaka kwa kila mtanzania , hivyo basi, kwa hizo dondoo za hapo juu inatosha kusema tujijengee utamaduni wa kuwekeza.

Kwa wale ambao tunapenda kuthubutu ni vyeme kuchukuwa hatua sasa, sababu kuanzia shilingi kama elefu kumi hivi unaweza kuanza kuwekeza kupitia mifuko ya UTT AMIS, kiasi hicho unaweza kukiona kidogo lakini ukishafungua akaunti yako UTT AMIS ni kama umejitengezea kibubu tena kibubu kinachotoa faida. Cha msingi ni kuhakikisha kuwa ukishapata akaunti yako jambo ambalo ni rahisi kabisa yaani ndani ya nusu saa baada ya kuwasiliana na UTT AMIS safari ya kuwekeza ina anza, hapo unatakiwa uwe unawekeza kiasi hicho au zaidi hakuna ukomo wa juu kadri uwezavyo. Ni vizuri ukajiuliza swali moja muhimu, ni hela gani ningeiwekeza lakini sikufanya hivyo, na je kama kile kilichokuwa kinafaa kuwekezwa kimewekezwa, nifanye nini nipate kiasi zaidi cha wekeza. Wekeza haba na haba hujaza kibaba. Na ukishawekeza usiwe na tamaa ya kupunguza uwekezaji wako mara kwa mara kwani muda unavyokuwa mrefu ndiyo katika hali ya kawaida faida inyokuwa nzuri. Unashauriwa kupunguza Uwekezaji wako kwa sababu maalumu tu.

Cha muhimu ni upime malengo yako dhidi ya muda, jambo lingine tukiwekeza tuhakikishe uwekezaji uwe wa kudumu yaani hata sisi tukitoweka tuvirithishe vizazi. Itakuwa ni mawazo potofu tukiwa wabinafsi. Ni kama yule anayesema sihitaji nyumba itakayo dumu zaidi ya miaka 70 kwani sitarajii kufika huko, kama ni watoto nishawasomesha wata fute vyao haya ni mawazo hasi , hayajengi.

Mifuko ya UTT AMIS ina malengo tofauti, mfano mfuko wa umoja lengo lake kubwa ni kukuza mtaji, wakati ule wa wewekeza ni huduma za bima zikiambatana na faida za Uwekezaji, mfuko wa watoto ni kwa ajili ya elimu au mtaji kwa watoto wamalizapo shule, mfuko wa kujikimu ni kwa wale wanaotaka kipato cha mara kwa mara kama vile wastaafu na mfuko wa ukwasi kipato cha wastani kwa muda muda mfupi.

Mbinu za kuweza kudumu sokoni

Kwa zaidi ya miaka 15 UTT AMIS imekuwa ikibuni na kusimamia mifuko ya uwekezaji wa pamoja, anzia mfuko wa Umoja 2005,      Wekeza Maisha 2007, Watoto 2008, Jikimu 2008 na Ukwasi 2013. Kwa kipindi chote hiki UTT AMIS imesaidia watu wa kipato cha chini, kati na juu kuongeza thamani katika mali zao (pesa), Mfuko wa umoja zaidi ya mara 9.6 ndani ya miaka 15, Wekeza Maisha zaidi ya mara 5 ndani ya miaka 12, Watoto zaidi ya Mara 4 ndani ya miaka 12, Jikimu gawio asilimia 2.5-4 kila robo mwaka huku thamani ya mtaji ikiongezeka na Ukwasi zaidi ya mara 2.7 ndani ya miaka 7. Kwa uhakika huu ni uwekezaji wenye faida sana.   Mfuko wa Ukwasi ulianza mwaka 2013 kipande kikiwa shilingi 100 leo hii kipande cha mfuko huo ni shilingi 272

Kwa kuanza si lazima uwe na pesa nyingi, unaweza anza kwa pesa kidogo tu, halafu ukawa unaongeza mara kwa mara na hii ni muhimu sana kwa wawekezaji wadogo ki umri, kwana mwekezaji anakuwa na ki umri na ki uwekezaji. Kumbuka muda ni muhimu ili kuleta faida.  Ukianza kupata kipato anza hapo hapo kutenga asilimia fulani kwa kwa ajili ya kuwekeza ili kikusaidie siku za baadae.

1 comment:

Pages