HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 29, 2021

Utepe Mweupe waomba wakunga wenye taaluma moja ya ukunga


MRATIBU wa Taifa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama  Tanzania  ' White Ribbon' Rose Mlay  akizungumza na waandishi wa habari.

 

NA ASHA MWAKYONDE

MRATIBU wa Taifa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama  Tanzania  ' White Ribbon' Rose Mlay amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan  kuwapatia akina mama wakunga wenye stadi za ukunga kama ilivyo kwa nchi nyingine zilizoendelea.

Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam jana wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi Mratibu huyo alisema katika nchi nyingine zilizoendelea zina wakunga ambao wafanya kazi moja tofauti na uuguzi.

Mratibu huyo alisema mtu asomee taaluma  ya ukunga tu na kwamba asiwe na kazi mbili kama ilivyo sasa mkunga anafanya kazi mbili pamoja na uuguzi.

" Huwezi kwenda kufanya kazi kwenye kuuguza pia ufanye kazi ya ukunga stadi lazima itashuka haitakuwa na ubora: Aliongeza.

Tumuheshimu mwanamke, tumuonee huruma tumpe mkunga ambaye atafanya kazi ya ukunga kama ilivyo kwa wataalamu wa meno,, wa dawa , awe ni  mkunga asiye na taaluma  nyingine," alisema Mlay.

Alisema inawezekana kwa sababu tayari walishazungumza na serikali  ambapo ilisikia na kuweka kozi ya diploma ya juu ya mkunga.

Mratibu huyo aliongeza kuwa Kuna wakunga ambao ambao wamesomea degree ya kwanza waendelee kusoma ya pili hadi kufikia PHD.

Alisema nchi nyingine zimeweza kuokao maisha ya mama kwa kuhakikisha kwamba hakuna mwanamke anayepoteza maisha kwa kukosa huduma ya kitaalamu  mfano nchi ya Sudani.

Mlay alieleza kuwa nyingi za kiafrika kama vile Malawi wanahakikisha  wakunga wanasomea ukunga na waunguzi wanasomea uuguzi.

" Kama Rais Mama  Samia akifikiria kutayariasha walimu kwa  sababu  huwezi kuwa na wakunga wafundishwe na mtu ambaye hana taaluma ya ukunga.

Tutayarishe walimu kuwe na chuo cha kuwafundisha wakufunzi ambao watawafundisha wakunga wengine,"alisema.

Aliongeza kuwa hapa nchini kulikuwa na chuo cha kufundishia wakunga wauguzi lakini chuo hicho kimefungwa.

No comments:

Post a Comment

Pages