HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2021

Profesa Ndalichako aongoza wadau kutoa maoni maboresho ya mitaala

 


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako, akifungua mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba, akizungumza katika mkutano wa kupokea maoni ya Wadau kuhusu Uboreshaji wa Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Benadeta Kiliani akizungumza katika mkutano huo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mifumo ya TEHAMA, Christian Mtavangu alipotembelea banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako, akiwa katika banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Wadau wa elimu wakiwa katika mkutano huo.

 
Na Irene Mark

WADAU wa elimu zaidi ya 700 wamekutana jijini Dar es Salaam leo Juni 18, 2021 kwa ajili ya kujadili na kutoa maoni ya kuboresha Mitaala ya Elimu kwa shule zote za Awali, Msingi na Sekondari hapa nchini.

Uboreshaji wa mitaala hiyo ni jukumu la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako amewataka wadau wa elimu walioshiriki kongamano hilo, kutoa maoni bora ili elimu ya Tanzania iwe yenye manufaa kwa mhitimu na taifa kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari.

Amesema uamuzi wa kuboresha mitaala hiyo umetokana na kukua kwa maendeleo na mabadiliko ya dunia huku akisisitiza kwamba serikali imezingatia pia malalamiko ya wadau.

“Mimi niwaombe tu muwe huru katika kutoa maoni kwa sababu yatasaidia katika kufanya elimu yetu kuboreka na kupata wahitimu tunawataka ambao watamaliza shule wakiwa na ujuzi wao tayari.

“Hii ni mara ya sitaa sasa nchi hii tunafanya mabadiliko ya mitaala ndio maana tunawasisitiza wadau wetu nyie mtoe maoni yanayofaa kwa mustabali wa elimu yetu kupitia mitaala hii tunawapika wasomi wa siku zijazo,” amesema Profesa Ndalichako.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, vilio vya wadau kuhusu maboresho ya mitaala
ni vingi kila kona na kwamba serikali imevisikia na kufanyia kazi hivyo wanapaswa kushiriki kikamilifu kwenye kutoa maoni yao.

“Tunataka mitaala ikajibu kiu ya watanzania maana tumesikia kilio cha kuboresha mitaala kuanzia bingeni, mitandaoni na hata kwenye mikutano na makongamano yanayohusu elimu... na hili lina maana kubwa kufanyika chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan,” amesisitiza Profesa Ndalichako.

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba amesema wanatarajia kwamba wadau watapata uelewa wa pamoja kuhusu maboresho ya mitaala hiyo ili watoe maoni yenye tija kwa elimu yetu.

“Na imani kuwa tutapata maoni mengi yatakayoboresha Elimu yetu nchini,hivyo tushirikiane kuhakikisha tunafanikisha ubora wa elimu yetu kwa watoto ambao ni viongozi wajao wa taifa hili,” amesema Dk. Komba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TET, Profesa Bernadetha Killiani, amesema taasisi hiyo umejipanga kuhakikisha inaboresha mitaala kuendana na mahitaji ya sasa na kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia.

1 comment:

  1. I strongly believe there are more fundamental problems in the education system besides curriculum. Let me try and say a thousand words using < 30 : Why is a primary school teacher paid less than a college lecturer? After what I have lived and gone through I am fully convinced it should be vice versa.

    ReplyDelete

Pages