Bondia Amir Khan kulia akimsukumizia konde zito mpinzani wake Carlos Molina
LOS
ANGELES, Marekani
“Baada ya Amir kumpiga Molina kulikuwa na
baadhi ya uvimbe mikononi, lakini hakuna sehemu yoyote ya mkono ama vidole
iliyovunjika. Lilikuwa jambo dogo lililotusukuma kumuona daktari na kuweka kila
kitu wazi”
BABA
mzazi wa bondia Amir Khan, Shah amezikata taarifa alizoziita za uongo kuwa
mwanaye huyo amevunjika mikono yote miwili - wakati alipokuwa akipambana na
kushinda Jumamosi dhidi ya Carlos Molina.
Tetesi
juu ya kuumia kwa kwa Khan zilisema kuwa, mkali huyo mzaliwa wa Bolton, yuko katika
hali mbaya akiuguza majeraha ya mikono yote miwili baada ya pambano hilo lililopigwa jijini Los Angeles, Marekani na kuongeza sasa yu
shakani kurudi ulingoni hapo Aprili mwakani.
Lakini
akionekana kukerwa na taarifa hizo, Shah baba wa mkali huyo jana amesema:
“Madai haya ni upuuzi uliovuka mipaka.
“Baada
ya Amir kumpiga Molina kulikuwa na baadhi ya uvimbe mikononi, lakini hakuna
sehemu yoyote ya mkono ama vidole iliyovunjika. Lilikuwa jambo dogo
lililotusukuma kumuona daktari na kuweka kila kitu wazi.
“Kama bondia hamalizi pambano kutokana na kupondeka kwa
mikono yake, labda hiyo inaweza kumnyima fursa ya kudhibiti makonde ya adui
yake ulingo — na walioona pambano lile watakubali kwamba Amir alipangua makonde
mengi tu ya Molina.”
Baada
ya kumdunda Molina na kumaliza mfululizo wa vichapo, Khan anatarajia kurejea
ulingoni hapo Aprili 13 — katiika pambano linaloweza kuwa dhidi ya Victor
Ortiz.
Wakati
huo huo, Kampuni ya Kimarekani inayompromoti Khan ya Golden Boy imejinasibu
kujaa matumaini ya kupata saini za mabondia watatu wa kufanya nao kazi.
Mabondia hao ni waliokuwa katika kikosi cha Uingereza kilichopata mafanikio
katika Olimpiki kiangazi jijini hapa.
Mkali
wa uzani wa 'Heavyweight' Anthony Joshua anaongoza orodha ya mabondia
wanaopigiwa hesabu na Golden Boy, pamoja na Anthony Ogogo na Luke Campbell.
Mkurugenzi
Mkuu wa Golden Boy, Richard Schaefer alikiri mchakato huo na kusema: “Binafsi
yangu natarajia kuwapa mikataba mabondia hawa na kuwaweka chini ya himaya yangu
na kuwalea ipasavyo.”
No comments:
Post a Comment