Pep Guardiola akiwa na Alex Ferguson
NEW YORK, Marekani
Mhispania
huyo ni chaguo namba moja la United kujaza pengo la Fergie, akifuatiwa na kocha
anayeinoa Real Madrid, Mreno Jose Mourinho, huku bosi wa Everton, David Moyes,
49, pia ni chaguo la Bodi ya Klabu pamoja na Ferguson mwenyewe
ALEX
Ferguson kwa mara nyingine jana amekutana na Pep Guardiola jijini hapa wiki
hii, huku kocha huyo wa zamani wa Barcelona
bado akisuasua kuamua juu ya hatima yake ya kurudi kufundisha soka.
Ferguson
Mskochi anayeinoa Manchester United, amepaa kwenda Big Apple akiwa na mkewe
Cathy kwa ajili ya mapumziko mafupi kuelekea Sikukuu ya Krismasi.
Lakini
Fergi akakutana na Guardiola — ambaye alishakutana naye mara mbili hapo kabla,
katika jiji hili - ambalo mabosi wote hao wanamiliki majumba ya kifahari ya
kuishi.
Haijawekwa
wazi kilichowakutanisha na kujadili, huku kukiwa na maswalia kama kocha huyo wa
United mwenye miaka 71 kama mwishoni mwa msimu
huu anaweza kutanua wigo wa kuendelea kubaki Old Trafford alikokaa kwa miaka 26
sasa.
Guardiola
anaweza kupatikana kujaza pengo la Fergie kutokana na ukweli kuwa hana timu,
huku akitajwa kuwa mlengwa namba moja wa klabu hiyo, ingawa pia wanafainali wa
msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich
na Chelsea
zimeripotiwa kumsaka kwa udi na uvumba.
Mhispania
huyo ni chaguo namba moja la United kujaza pengo la Fergie, juu ya kocha
anayeinoa Real Madrid Jose Mourinho, huku bosi wa Everton, David Moyes, 49, pia
ni chaguo la Bodi ya Klabu pamoja na Ferguson
mwenyewe.
Guardiola,
41, aliacha kuinoa klabu yake ya Barca mwishoni mwa msimu uliopita baada ya
kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya Hispania 'La Liga,' na mawili ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya - yote akiichapa United katika fainali.
Mourinho
anajiandaa kutimka Real Madrid kiangazi hiki, lakini watu wengi wanatambua
ukweli kuwa Old Trafford si miongoni mwa sehemu ambnazo anaziangalia kwa jicho
la kutamani kufanya kazi.
No comments:
Post a Comment