Kocha wa Chelsea, Rafael Benitez
YOKOHAMA,
Japan
“Watu uniuliza maswali kama ubingwa wa England kwa msimu huu ni mbio za farasi wawili
wa jiji la Manchester?.
Lakini ki-uhalisia, kwa pointi tatu kwa mechi moja, kama
unashinda mechi mbili au tatu mfululizo, unakuwa umejiongezea kujiamini”
WAKATI kesho Jumapili mchana wakishuka kwenye dimba la
International kuumana na Corinthians katika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia,
kocha wa Chelsea, Rafael Benitez, anaamini kikosi chake kinaweza kuzalisha
morali ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Ndoto za Benitez zinakuja wakati akikiongoza kikosi chake
kucheza fainali ya Dunia ngazi ya klabu dhidi ya Corinthians, huku vinara wa
Ligi Kuu Man United leo Jumamosi wanasaka ushindi wa kupanua wigo wa pointi zao
na Chelsea
kufikia 13.
Lakini Benitez anaamini kwamba kama wataibuka na ushindi
dhidi ya Corinthians ya Brazil
katika fainali ya kesho jijini hapa, utakuwa ujumbe mahususi kwa Alex Ferguson na
Roberto Mancini kuwa The Blues imerejesha rasmi nguvu za kuwania taji.
Benitez kocha wa zamani wa Liverpool anayeandamwa na
jinamizi la kutopendwa na mashabiki klabuni Stamford Bridge
tangu alipomrithi Roberto Di Matteo, alisema: “Kabla ya kuja hapa, nilikuwa
nasikia ofa kibao za kunihitaji kufanya kazi na klabu tofauti.
“Ningeweza kupata na kufanya kazi katika nchi za Hispania au
Italia, ama China,
na kupata pesa kubwa ya mshahara katika klabu kwa miaka 10. Lakini nilikuwa
nasubiri kikosi cha daraja la juu. Nataka kushindana kutwaa mataji.
“Watu uniuliza maswali kama ubingwa wa England kwa msimu huu ni mbio za farasi wawili
wa jiji la Manchester (Man United na Man City)?.
Lakini ki-uhalisia, kwa pointi tatu kwa mechi moja, kama
unashinda mechi mbili au tatu mfululizo, unakuwa umejiongezea kujiamini.
“Kama tutashinda na kutwaa ubingwa wa dunia ngazi ya klabu hapa
na tukacheza kama tulivyocheza katika nusu
fainali Alhamisi, huku tukiboresha kiwango chetu kwenda mbele kwa uwiano sawa, tunaweza
kurejea katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu.
“Kiasi cha mechi ngapi? Mimi sijui hilo. Wengine wanaweza kufanya hivyo pia. Lakini
baada ya ushindi wa mechi tatu au nne katika kinyang’anyiro, kujiamini kwetu
kunaweza kuwa juu. Sasa kwa nini isiwezekane,? Alimaliza Benitez kwa swali.
No comments:
Post a Comment