Rais wa Klabu ya Olympique Lyon, Jean-Michel Aulas
PARIS, Ufaransa
"Hatuwezi kufikiria kuhusu kushindana na PSG kuwania
ubingwa. PSG inatutisha mno sisi. Itakuwa ni kosa kutowahofia kocha Carlo
Ancelotti na Mkurugenzi wa Michezo Leonardo, huku timu yao ikishinda kwa kishindo katika mechi zao
kwa mabao 4-0"
MAHASIMU wa Paris St Germain, wamekiri kuwa klabu hiyo
tajiri zaidi katika Ligi Kuu ya hapa itaibuka mabingwa wa Ligue 1 mwishoni mwa
msimu na kinachofanywa na klabu nyingine ni kuchelewesha taji, kocha wa Olympique Lyon Remi Garde ameyasema hayo juzi
usiku.
Kauli ya kocha wa Lyon imekuja wakati kikosi chake
kikijiandaa kushuka ndani ya Uwanja wa Parc des Princes kesho Jumapili, huku PSG
ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 32, tatu nyuma ya wageni
wa pambano la leo Lyon.
Hii ina maama kama wenyeji watashinda nyumbani, Lyon
watashushwa chini kwa uwiano wa mabao kama, ambapo Garde alisema mechi hiyo ni
muhimu: "Mchezo huu ni uhimu, lakini sio muhimu sana.
"Kuna nafasi nzuri wakati wote tunajua tayari kwamba
bingwa wa ligi atakuwa nani mwishoni mwa msimu, ingawa sisi ni miongoni mwa
tunaotamani ubingwa huo kwa muda mrefu kama
tunaweza kufanya hivyo.
"Ndio, tutajaribu kadri tuwezavyo. Sisi tuko hapa kwa
ajili ya jambo hilo
– kujaribu kuwaudhi kwa kuwatibulia."
Licha ya kukalia kilele cha Ligue 1 kwa wiki kadhaa sasa,
Lyon inaifuata PSG ikiwa na hofu ya kiwango bora ilichonacho klabu hiyo chini
ya wamiliki wa Qatari –wakiibuka na ushindi mnono mfululizo wa mabao 4-0 katika
mechi mbili zilizopita dhidi ya Evian na Valenciennes.
"Hatuwezi kufikiria kuhusu kushindana na PSG kuwania
ubingwa. PSG inatutisha mno sisi," hiyo ni kauli ya raidi wa Lyon, Jean-Michel
Aulas akiliambia gazeti la kila siku la Le Parisien la nchini hapa.
"Itakuwa ni kosa kutowahofia (kocha) Carlo Ancelotti na
(Mkurugenzi wa Michezo) Leonardo, huku timu yao ikishinda kwa kishindo katika mechi zao
kwa mabao 4-0," alisisitiza Rais wa Lyon, Aulas.
No comments:
Post a Comment