Adam Robert akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi alivyotekwa na kukatwa viganja vya mikono
Daktari mstaafu wa hospitali ya mkoa wa Geita, Patrick Bulugu,
akionesha kiganja bandia cha mkono wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Adam
Robert (13), aliyerejea kutoka nchini Canada jana, ambako alipatiwa matibabu ya
viungo vilivyokatwa kwa imani ya kishirikina. Adam alipata matibabu kwa msaada
wa Shirika la Under the Same Sun.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MTOTO Adam Robert (13) mwenye ulemavu wa ngozi jana amerejea
nchini akitokea Canada alipokuwa akipatiwa matibabu ya viungo vilivyokatwa na
watu kutokana na imani za kishirikina.
Mtoto huyo ambaye alifanyiwa unyama huo mwaka jana akiwa nyumbani
kwa wazazi wake ambaye mmoja ni mama wa kambo 'steps mother' aliweza kusaidiwa na
Shirika la Under the Same Sun linalohudumia watu wenye ulemavu wa ngozi nchini
hadi kupata unafuu na kurejea nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Robert alisema mara baada
ya kupatiwa matibabu kwa sasa anajisikia vizuri na kwamba anaweza kuendelea na
shule.
Robert ambaye alikatwa vidole viwili na nusu ikiwa ni cha gumba na
cha shahada huku cha kati kikiwa kimekatwa nusu alishindwa kuendelea na shule
kutokana na kukosa uwezo wa kuandika kwa kuwa alishindwa hata kushika kalamu.
Kwa mujibu wa Dk.Patrick Burugo aliyekuwa akimpa matibabu Geita na
hatimaye kwenda naye nchini Canada kwa msaada wa shirika la Under the Same sun
alisema matibabu yake yalikuwa makubwa na ya hali ya juu,mbapo ilimlazimu
kutolewa kidole gumba cha mguuni na kuwekwa mkononi.
Dk. huyo aliyendelea kueleza kuwa Robert alilazwa katika hospital
ya Voncouver ambapo upasuaji wake ulidumu kwa zaidi ya saa 13 ambapo kuna
wakati madaktari bingwa wa upasuaji walilazimika hata kutoa misuli sehemu
nyingine ya mwili na kuunga katika kidole hiko ili mradi kiweze kupata
mawasiliano na kiweze kufanya kazi kwa haraka.
"Tumefanya upasuaji kwa zaidi ya saa 13 ambapo ilibidi kidole
cha mguu gumba kitolewe mguuni na kiwekwe katika mkono na kipande cha nyama
kukatwa kwenye paja na kuungwa mkononi kwa kweli matibabu yalikuwa ni ya hali
ya juu sana,"alisema Dk.Burugo.
Hata hivyo mtoto huyo alitoa ushuhuda wake ambapo alisema hataki
kurudi tena nyumbani kwa wazazi wake hao akihofia maisha yake kuwepo hatarini.
Alielezea tukio zima huku akieleza kuwa akiwa nyumbani kwao
alikuja mgeni ambaye alikaribishwa na mama wa kambo pamoja na baba yake mzazi
ambapo walimtuma kama mara mbili ndani chumvi na moto.
lieleza kuwa wakati wakiwa wanamtumna aliweza kufanya kazi zote
hzio lakini baada ya kufika kwa muda wa kulala walimwita atoke nje na ndipo
yule mgeni aiyemjua jina kuanza kumkata kata vidole na sehemu mbalimbali ya mwili.
Alisema wakati akiwa anafanyiwa vitendo hivyo baba na mama ake
walikuwa pembeni lakini yeye katika kujihami aliamua kum'ngata mtu huyo sehemu
zake za siri na ndipo akamuachia.
"Nilimng'ata sehemu za siri akaniachia mara moja na ndipo
baba akampigia simu baba mkubwa akaja nikapelekwa hospitali kwa kweli nilipatwa
maumivu sana sana,"alisema Robert.
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Vicky Mtekema alisema ni furaha
kubwa kwa mtoto Robert kurudi mzima huku akiwataka watanzania kuacha kufanya
vitendo hivyo vya kinyama kwa watu hao.
Naye Rais na Mwanzilishi wa shirika hilo Peter Ash aliitaka jamii
ya Tanzania kuungana pamoja ili kuweza kupinga ukatili huo ambao unatokana na
imani za kishirikina kwa kisingizio kwamba wanaweza wakapata madini mengi na
kuwa matajiri jambo ambalo si kweli.
No comments:
Post a Comment