WIZARA ya Afya na
Ustawi wa Jamii inatarajia mwaka ujao kuanzisha chanjo mpya mbili za
pneumococcal na rotavirus, ambazo ni maalum katika kukinga maradhi na vifo kwa
watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam leo, na
Mkurugenzi wa Kinga, Elias Chinamo, wakati wa warsha ya siku moja ya wandishi
wa habari, ya kuwajengea uwezo wa kufilisha elimu sahii kwa jamii pamoja na
kuihamasisha jamii kuhusu chanjo hizo mpya,
zitakapoanza mwaka 2013.
Alisema walengwa wa chanjo hizo watakuwa ni watoto
waliyonaumri wa chini ya miezi 12 ambapo chanjo ya kukinga nimonia (pcv13),
itatolewa mara tatu kuanzia umri wa wiku sita, 10 na 14.
Chinamo akubainasha kuwa chanjo ya kinga ya kihara (rotavirus), itatolewa mara mbili kuanzia
imri wa wiku sita na 10, inasisitizwa kuwa ili mtoto apate kinga lamili ni
lazima akamilishiweratiba mapema.
Alisema kitaalam zinaonesha kuwa chanjo ya ‘pneumococcal’
hukinga maambukizi ya nimonia kwa asilimia 38, homa ya uti wa mgongo kwa
takriban asilimia 87; na chanjo ya ‘rotavirus’ hukinga kuharisha kuharisha
kunakosababisha vifo vya watoto kwa aslimia 80.
Chinamo aliongeza kuwa
kwa sehemu kubwa hukinga ugonjwa wa kuharisha unaosababshwa na vimelea
vya aina nyungune pia.
Alibainisha kuwa vimelea ‘Streptococcus pneumonie’ ni
kisababishi kikuu cha maradhi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa nimonia na homa
ya uti wa mgongo kwa watoto katika nchi zinazoendelea.
Aidha, vimelea vya ‘rotavurus’ kwa upande mwingine
husababisha takriban asilimia 80 ya maradhi na vifo vitokanavyo na kuharisha
kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano duniani
Vile vile alitoa wito kwa wananchi kuwa channjo hizo ni
salama na zitatolewa bure bila malipo ambapo pia aliwahakikishia wananchi hao
kuwa chanjo zitatolewa na wataalam wenye
uzoefu.
No comments:
Post a Comment