Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
akipozi na kikosi kizima cha michezo mbalimbali cha Ikulu Sports Club ambacho
kilinyakua jumla ya makombe matano katika michezo mbalimbali ya Shirikisho la Michezo ya Wizara (SHIMIWI) mwaka
huu mjini Morogoro. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi na
kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore katika
hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika
leo Deswemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo
iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla
ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo
wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza
katika michezo ya Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume
na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo
ya makombe matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI
ya maka huu mjini Dodoma katika hafla ya kukabidhi
makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012
Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia
Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500
kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91
wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya
Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume na kushik nafasi
ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha
na Bw. Miraji Ahmed Saleh ambaye ameibuka kuwa mfanyakazi Bora na Hodari kwa
mpigo, akiwa kama Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za Ikulu na
Zahanati katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia
wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es
salaam
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu
Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Huduma
za Ikulu Bw Julius Mogore (wa pili kushoto ) pamoja na mwenyekiti wa
TUGHE tawi la Ikulu Bw. Paulo Mgeni (kulia) wakiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie
Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu
Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo (Taifa
Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba
17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa na Mwadawa Twalibu,
Sophie Komba na Pascalia Kibayasa wachezaji wa netball wa Ikulu
Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Queens) ya mchezo
huo kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi bora wa Ofisi ya Rais, Ikulu katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Naibu
Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi akiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie
Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball
ya Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo
(Taifa Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo
Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue akimpa zawadi Bw. Miraji Ahmed Saleh kwa kuibua mfanyakazi
bora na pia mfanyakazi hodari wa Ofisi ya Rais Ikulu. Bw Saleh
ni Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za
Ikulu na Zahanati katika hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17,
2012 Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment