HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 26, 2013

Chakula cha Jioni kwa Ujumbe wa Oman


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,na Mawaziri wengine walipoungana katika hafla ya chakula  maalum kwa ujumbe wa wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa na Waziri Yussuf bin Alawi bin Abdullah,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman,Yussuf bin Alawi bin Abdullah,akichukua chakula wakati wa hafla maalum kilichoandaliwa  kwa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa na Waziri Yussuf,katika
Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar/


 Baadhi ya Viongozi wa Ujumbe wa Nchini Oman na Viongozi wa Taasisi mbali mbali hapa Zanzibar wakiwa katika  hafla ya chakula  maalum kwa ujumbe wa wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa
na Waziri Yussuf bin Alawi bin Abdullah,(hayupo pichani) katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.
Viongozi  wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,waliojumuika na ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,wakichukua chakula wakati wa hafla maalum kilichoandaliwa  kwa ujumbe huo,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,(kushoto) alipokuwa akitoa hutuba fupi ya kuwashukuru wageni  wa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,ulioongozwa na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman  Yussuf bin Alawi bin Abdullah,(kulia) baada ya kushiriki katika  hafla ya chakula maalum,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini,(kulia)  akimkabidhi zawadi ya Kasha  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman  Yussuf bin Alawi bin Abdullah,akiwa kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman,baada ya hafla ya chakula maalum,kilichoandaliwa kwa ujumbe huo,katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman  Yussuf bin Alawi bin Abdullah,akitoa hutuba fupi ya  shukururani zake kwa kuandaliwa chakula  maalum,akiwa na ujumbe wake katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages