HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 27, 2013

NMB KINARA WA UBORA 'SUPERBRANDS' KATIKA TAASISI ZA FEDHA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB Iman Kajula  akipokea Tuzo ya Superbrands kutoka kwa Mkurugenzi wa Superbrands  Afrika Mashariki, Jawad  Jaffer wakati wa hafla za kuwakabidhi washindi wa tuzo hizo na benki ya NMB imekua mshindi katika Taasisi za Kifedha Tanzania. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing (katikati) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB Iman Kajula (kushoto) na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo ya Superbrands.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB Iman Kajula. 
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano NMB Iman Kajula  akiteta jambo na  Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing


DAR ES SALAAM, Tanzania

BENKI ya NMB imeibuka kinara wa tuzo za Ubora wa Makampuni ‘Superbrands 2013/14’ kwa upande wa Taasisi za Kifedha nchini, huku ikiahidi kuboresha utendaji wao na sasa wateja watapata huduma popote walipo bila kwenda kwenye matawi ya benki hiyo.

Akizungumza leo wakati wa hafla ya kupokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Superbrands, Afrika Mashariki, Jawad Jaffer, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa NMB, Iman Kajula alisema kwao ni zaidi ya fahari kwa kuwa kinara wa Superbrands kwenye sekta ya fedha.

Ushindani wa katika taasisi za kifedha, nia ya dhati ya kusadia ukuzaji maendeleo kwa wateja wake na kuendelea kuwa kinara wa miongoni mwa makampuni bora kwa huduma, yanaisukuma NMB kuhamishia huduma za kibenki katika simu za mikononi za wateja wao na Watanzania kwa ujumla.

“NMB inajisikia fahari kubwa kuwa kinara wa ‘Superbrands’ katika sekta ya fedha na ili kujiweka juu zaidi, tumepania kupunguza msongamano kwenye matawi yetu kwa kuhamishia huduma za kibeki katika simu na kuharakisha harakati chanya za maendeleo,” alisema Kajula.

Aliongeza kuwa, kwa miaka sita sasa NMB imepanua wigo wa maendeleo yake na wateja kwa ujumla, ambapo kwa sasa ina zaidi ya matawi 148, ATM 500, wakiwamo pia wateja wanaotumia simu za mkononi ‘NMB Mobile’ zaidi ya 800,000 na huduma mbadala kama Internet Banking Call Center.

No comments:

Post a Comment

Pages